SERIKALI YATUMIA SHILINGI BILIONI 187 KWA MATIBABU YA WAZEE

 Mwandishi Wetu,

Serikali imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 661 kwa ajili ya msamaha wa matibabu kwa makundi maalum, ambapo Shilingi Bilioni 187 zinatumika kugharamia matibabu ya wazee wasiochangia katika Mfuko wa Bima ya Afya.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ya Mwaka 2023, ambayo inalenga kuhakikisha makundi maalum, yakiwemo wazee, yanapata huduma za afya bila vikwazo vya kifedha.

“Serikali inatambua mchango wa wazee katika jamii na umuhimu wa kuhakikisha wanapata matibabu bora. Kati ya shilingi Bilioni 661 zilizotengwa kwa msamaha wa matibabu, Shilingi Bilioni 187 zimeelekezwa mahsusi kwa wazee wasio na uwezo wa kuchangia kwenye mfuko wa bima,” amesema Dkt. Mollel.



Post a Comment

Previous Post Next Post