TANZANIA YASHIRIKI KIKAO CHA KANDA YA AFRIKA WHO



Mratibu wa Afrika wa Masuala ya Afya katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, ambaye pia ni Mwambata wa Afya wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Geneva, Dkt. James Kiologwe, ameongoza kikao cha Kanda ya Afrika cha nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kinachofanyika wakati wa Mkutano wa 156 wa Bodi ya WHO unaoendelea jijini Geneva, Uswisi.

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na utaratibu wa kuziba pengo la kibajeti lililosababishwa na kusudio la Marekani kujitoa katika Shirika hilo.




Post a Comment

Previous Post Next Post