BENKI KUU YA TANZANIA YATOA ELIMU CHUO CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST)

 

Wanachuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST)wakiangalia noti bandia katika mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu Tanzania Tawi la Mbeya

Akitoa elimu kwa Wanachuo na Wafanyakazi na Wahadhiri Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST)Nicholous Kesi Daktari wa Uchumi Idara ya Uchumi Tawi la Mbeya amesema zoezi hilo ni endelevu lengo jamii iweze kuzifahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Benki Kuu.

 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia(MUST)Profesa Godliving Mtui amesema mafunzo waliyoyapata yamewajengea uwezo wa kuilewa Benki Kuu.Aidha amesema bado kuna uhitaji mkubwa wa elimu ya fedha hususani masuala ya fedha mtandao.

 Sweetlet Mushi – Afisa Mkuu Mwandamizi wa Benki Kuu Tanzania Tawi la Mbeya akionesha Wanachuo MUST Mbeya fedha zilizochakaa au kukunjwakunjwa  zikiwa zimeharibiwa kwa utaratibu maalum na Benki

 Joyce Sama – Ofisa Msaidizi Benki Kuu. akitoa somo la kutambua alama za usalama zilizopo katika Noti  na njia sahihi za utunzaji wa Noti na Sarafu. kwa wanachuo wa MUST Mbeya

 Pamela Kombe – Mhasibu Mwandamizi Benki Kuu akielezea kuhusu namna Benki Kuu ya Tanzania inavyofanya Usimamizi wa Taasisi za Fedha nchini.

Sungura Mashini – Meneja Msaidizi wa Uchumi Benki Kuu Tawi la Mbeya  akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa Benki hiyo katika kukuza uchumi wa Tanzania

Petty Ndowo – Afisa Mkuu Benki Kuu  Akiwaonesha Wanachuo wa MUST Kifaa ambacho kinatumika kutambua noti bandia na halali.

vWanachuo Chuo Kikuu  MUST Mbeya wakifanya utambuzi wa noti halali na bandia katika mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu Mbeya

 Benki Kuu  ya Tanzania Tawi la Mbeya limeendelea kutoa elimu kwenye makundi mbalimbali ili jamii iweze kuzitambua shughuli zinazofanywa na Benki Kuu nchini.

Akitoa elimu kwa Wanachuo na Wafanyakazi na Wahadhiri Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST)Nicholous Kesi Daktari wa Uchumi Idara ya Uchumi Tawi la Mbeya amesema zoezi hilo ni endelevu lengo jamii iweze kuzifahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Benki Kuu.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia(MUST)Profesa Godliving Mtui amesema mafunzo waliyoyapata yamewajengea uwezo wa kuilewa Benki Kuu.

Aidha amesema bado kuna uhitaji mkubwa wa elimu ya fedha hususani masuala ya fedha mtandao.

Hata hivyo amesema jamii hususani wanachuo mbali ya fani wanazosoma chuoni wanapaswa kujifunza sana mambo mengine kama ya fedha ili wasijiingize kwenye mikopo isiyo na tija hivyo kujikuta wanashindwa hata kulipa ada.

Magreth Giga mhadhiri msaidizi amesema elimu waliyoipata itawasaidia kwenye jamii husani utambuzi wa alama kwenye fedha na utunzaji wa fedha sambamba na kufahamu mifuko ya fedha na kujua thamani ya fedha.

Gaudence Mlelwa amesema kupitia elimu hiyo amejifunza namna ya utunzaji fedha na masuala ya uwekezaji hususani baadhi ya kampuni zisizosajiliwa kufanya shughuli za kifedha ambazo huishia kuwatapeli wananchi.

Benki Kuu Tawi la Mbeya limekuwa likitoa elimu kwa makundi mbalimbali kama wafanyakazi,wafanyabiashara,wakulima,wachimbaji na wanavyuo ili kuepusha utakatishaji wa fedha pia kuzuia matumizi ya fedha bandia ambazo zikiingizwa kwenye mzunguko wa fedha zitasababisha mdororo wa kiuchumi.

Post a Comment

Previous Post Next Post