MHE BALOZI DKT CHANA: ELIMISHENI WANANCHI WASICHOME MISITU




                            ……….,……………

Na Sixmund Begashe wa MNRT

Waziri wa Maliasili na Utalii ameuagiza uongozi wa mradi wa Panda Miti kibiashara ( PFP 2) mkoani Iringa uongeze kasi ya kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kutochoma misitu ili kuhifadhi rasilimali hiyo.

Waziri Balozi Dkt. Chana ameyasema hayo Mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi kwenye ofisi za Mradi kukagua utekelezaji wa programu mbalimbali za uhifadhi wa Misitu.

Mhe Balozi Dkt. Chana amesema Taifa limekuwa likipata hasara kubwa inayotokana na uchomaji wa Misitu hivyo ushiriki wa Taasisi binafsi katika kuelimisha jamii juu ya madhara ya moto kwenye misitu ni muhimu sana.

Mradi wa Panda Miti Kibiashara unajishughulisha na upandaji miti na kuhamasisha wananchi kupanda miti kibiashara katika mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma.

Post a Comment

Previous Post Next Post