WAZIRI BALOZI DKT. PINDI CHANA AWEKA KAMBI MLIMA KILIMANJARO




                            ……………………..

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameweka Kambi katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikiwa ni mwendelezo wa ushiriki wake kuhakikisha moto unaowaka  katika maeneo machache yaliyosalia katika hifadhi ya Mlima huo.

Akiwa katika hifadhi hiyo Waziri Balozi Dkt. Chana amepokea taarifa ya utekelezaji wa kazi inayoendelea ya kuzima moto  akiwashukuru na kuwapongeza  wadau wote waliojitolea kwa hali na mali katika kuhakikisha moto unadhibitiwa katika maeneo yote.

Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana ameendelea kukemea vikali tabia ya  baadhi ya wananchi  wanaoanzisha au kuchoma moto hovyo katika maeneo yaliyohifadhiwa na kuisababishia Serikali na wananchi wake hasara kubwa  akisisitiza  kuwa yeyote atakayebainika atafikishwa kwenye vyombo vya Sheria.

“Huu ni msimu wa maandalizi ya kilimo, natoa rai kwa ndugu zangu wakulima mnaopakana na Hifadhi za Taifa muwe makini pindi mnaposafisha mashamba yenu, msitumie  moto bali tafuteni njia mbadala ili kuepusha moto kuchoma Misitu na kusababisha hasara kubwa, yeyote atakayesababisha moto kwenye Hifadhi za Taifa atachukuliwa hatua kali za kisheria”. Amesisitiza Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana

Post a Comment

Previous Post Next Post