Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,(Sera,Bunge na Uratibu) George Simbachawene,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na muongozo wa matumizi ya matokeo hayo leo Oktoba 28,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamza Hassan Juma,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na muongozo wa matumizi ya matokeo hayo leo Oktoba 28,2022 jijini Dodoma.kushoto ni Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,(Sera,Bunge na Uratibu) George Simbachawene
………………
Na Alex Sonna-DODOMA
Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,(Sera,Bunge na Uratibu) George Simbachawene,amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kutangaza Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na muongozo wa matumizi ya matokeo hayo.
Hayo ameyasema amesemwa leo Oktoba 28,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema kuwa Oktoba 31,2022 historia itaandikwa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma
Waziri Simbachawene amesema kuwa uzinduzi huo ni tukio muhimu katika historia ya maendeleo ya nchi ndio maana Serikali imeamua kuhakikisha kunakuwa na uwakilishi wa wananchi wa makundi yote ili waweze kushiriki katika tukio hili la kihistoria.
“Oktoba 31 ni siku maalum kwa taifa letu hivyo basi hatuna budi kuhakikisha kwa tuliopo Dodoma na mikoa ya jirani tunajitokeza kwa wingi uwanja wa Jamhuri na wale tutakaokuwa mbali tufuatilie uzinduzi huo kupitia vyombo vya habari ili tushiriki pamoja na Mheshimiwa Rais kujua tupo wangapi wakati atakapotangaza Matokeo hayo ya Mwanzo,”amesema
Simbachawene amesema kuwa katika zoezi hilo wegeni wengine ni pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Marais hao wastaafu watatunukiwa tuzo maalum kwa kufanikisha Sensa katika vipindi vya uongozi.
“Sensa ya Watu na Makazi hufanyika mara moja kila baada ya miaka kumi na matokeo yake ndio yanayotumika katika kufanya maamuzi yote muhimu yanayohusu maendeleo ya nchi kwa kipindi cha miaka kumi hadi Sensa nyingine,hivyo
Na kuongeza kuwa “Sherehe hizi za uzinduzi wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 zitahudhuriwa na viongozi wote wakuu wa Serikali pamoja na Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Marais wastaafu wa Zanzibar,”amesema Simbachawene
Amewataja baadhi ya Wageni watakaoshiriki katika Uzinduzi huo kuwa ni viongozi wa Serikali wakiwemo mawaziri na manaibu waziri, Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Serikali zetu zote mbili, Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar, viongozi wa vyama vya Siasa na wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii.
“Wageni wengine mashuhuri ni pamoja na Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao humu nchini, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa yakiwemo ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika na Wadau wengine wa Maendeleo,”amefafanua Simbachawene.
Amewataja baadhi ya Wageni watakaoshiriki katika Uzinduzi huo kuwa ni viongozi wa Serikali wakiwemo mawaziri na manaibu waziri, Makatibu wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Serikali zetu zote mbili, Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar, viongozi wa vyama vya Siasa na wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii.
“Wageni wengine mashuhuri ni pamoja na Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao humu nchini, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa yakiwemo ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika na Wadau wengine wa Maendeleo,”amefafanua Simbachawene.
Aidha amesema katika sherehe hizo, mbali ya kuzindua Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan atazindua pia Mwongozo Maalum wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ambao lengo lake kuu ni kuhakikisha matokeo ya Sensa yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Matokeo haya ni muhimu sana kwa makundi yote katika jamii, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji na hasa kwa Serikali yetu inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwani Serikali itaweza kupanga mipango yake kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kulingana na idadi, mahitaji na mazingira wanamoishi,”amesisitiza na kuongeza;
Kwetu sisi wananchi wa Dodoma, hii itakuwa historia kwa kuwa itakuwa mara ya kwanza kushuhudia tukio la uzinduzi wa Matokeo ya Sensa ambao ni fursa moja muhimu kwenu kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia uzinduzi huo ambao utapambwa na kila aina ya shamrashamra kuonesha kuwa sio tu kuwa ni tukio la kihistoiria kufanyika Dodoma pia ni tukio linalitokea mara moja tu kila baada ya miaka kumi,”amesema.
Ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa jirani kujitokeza kushuhudia uzinduzi huo na wahakikishe wanafika majira ya saa 12 kamaili asubuhi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamza Hassan Juma amesema watakuwa na ujumbe wa watu zaidi ya 150 watakaoshiriki siku hiyo .
Juma amesema sensa ya mwaka huu ilifanikiwa kwa kiwango cha juu kwa sababu ya kuungwa mkono na viongozi wa kisiasa na kidini .