Kutokana na changamoto ya upatikanaji wa maji Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ametembelea mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo wilaya ya Kigamboni ili kuona ni kwa namna gani unaweza kupunguza makali ya upatikanaji wa maji kwenye Mkoa huo.
Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amesema ziara hii ya leo ni mwendelezo wa ziara aliyoifanya kwenye mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu na kueleza kwa uhalisia kuhusu hali ya maji kwenye vyanzo vya maji na kutoa ahadi kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji.
"Rais Samia alielekeza kwamba wakati tunapitia changamoto ya upatikanaji wa maji basi mradi wa maji wa Kigamboni ufanywe kwa haraka kwa kuwa ameidhinisha bilioni 25 ili kumaliza huu mradi na kupunguza changamoto ya upatikani wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam. Alisema Makalla
Pia amemtaka mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na kama asipomaliza kwa muda uliopangwa ataweza kuchukuliwa hatua stahiki kwani lengo kubwa ni kupunguza makali ya upatikanaji wa maji.
Pia amesema kisima kimoja kilichowashwa leo kitaweza kutoa huduma kwa wakazi wa Kigamboni hivyo vikiwashwa visima vingine vitaweza kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam kwani mkandarasi yupo kwenye kulaza mabomba ili kuweza kusambaza maji.
Makalla amefanya ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II pamoja na kuwasha pampu ya kisima kimoja kinachopeleka maji kwenye tanki la maji lenye ujazo wa lita milioni 15 litakaloweza kutoa huduma ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ameishukuru Serikali kwa kuiwezesha na kuisaidia DAWASA hasa kwenye kipindi hiki cha uhaba wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuitaka uendelee kuwa nao begakwabega mpaka watakapotatua changamoto ya upatikanaji wa maji.
Mwamunyange amesema DAWASA wataendelea kuimarisha miundombinu ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam kwani wakazi wa Mkoa huo wanaendelea kuongezeka kila kukicha hivyo hawezi kumaliza changamoto ya maji kwa asilimia mia moja .
Mradi huu ulianza kutekelezwa mwezi Disemba mwaka 2019 huku ukigharimu kiasi cha bilioni 24 fedha za ndani za Mamlaka na kukamilika kwakwe kutanufaisha wakazi 250,000 wa maeneo ya Kibada, Mjimwema, Masonga, Kimbiji, Mpera na maeneo ya karibu.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla(kulia) pamoja na wajumbe wa Bodi ya DAWASA wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja(kushoto) kuhusu moja ya kisima pamoja na pampu ya kusukumia maji wakati wa kuwasha pampu hiyo katika mradi wa maji wa Kisarawe II unaotekelezwa na DAWASA.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akiwasha pampu ya kisima cha kwanza kinachopeleka maji kwenye tanki la lita milioni 15 katika mradi wa maji Kisarawe II unaotekelezwa na DAWASA.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla pamoja na Bodi ya DAWASA wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mradi wa Kisarawe II walipotembelea Tanki la maji la Kisarawe II lenye ujazo wa Lita Milioni 15 linalojengwa na DAWASA na kuwasha moja ya kisima katika Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitolea ufafanuzi Tanki la maji la Kisarawe II lenye ujazo wa Lita Milioni 15 linalojengwa na DAWASA katika Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla pamoja na Bodi ya DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II pamoja na kuwasha pampu ya kisima kimoja kati ya Saba