Mhe. Gwajima - Shindano la Dunia la Urembo, Utanashati na Mitindo laitangaza Tanzania duniani

Na John Mapepele

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt, Doroth  Gwajima amesema  mashindano  ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaidia kuitangaza Tanzania duniani.

Mhe. Gwajima ametoa kauli hiyo leo kwenye  mashindano ya Dunia ya urembo, utanashati na  mitindo  linalofanyika  jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Amempongeza Mhe. Rais  kwa kutoa kipaumbele  kwenye michezo na kusisitiza kuwa  mashindano  haya ya michezo na utamaduni yanasaidia kuleta upendo, mshikamano na udugu  kwa mataifa mbalimbali.

Amewasihi wazazi wenye watoto walemavu kuwatoa watoto wapate elimu ili waweze kuonyesha  vipaji vyao badala ya  kuendelea  kuwaficha majumbani na kuongeza  kuwa sera ya utamaduni  1997 inaeleza  ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye utamaduni.“Hii imetuonesha kuwa sisi sote  ni sawa mbele za Mungu mimi naweza kuwa sina hiki  na wewe ukawa na  hiki” ameongeza Mhe. Gwajima

Amesema kupitia mashindano haya na onyesho la Filamu ya Royal tour waliyoitazama  watakuwa mabalozi wazuri wa  kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa  amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa  maelekezo  anayotoa kwenye  sekta anazoziongoza  ambapo kutokana na maelekezo hayo kumekuwa na mafanikio makubwa.


Amefafanua kuwa  wizara yake itaendelea kutafsiri na  kutekeleza  kikamilifu maelekezo yote yanayotolewa na Mhe. Rais na Serikali kwa ujumla.

Aidha amesema jukumu la Wizara yake ni kuleta furaha na Faraja kwa watanzania  na  kwamba  shindano hili ni mwendelezo wa  Royal Tour.Mhe Mchengerwa ametoa zawadi ya kinyago kwa Rais wa Dunia wa Mashindano hayo Bonita Lee.

Shindano hili limepambwa na wasanii mbalimbali waliotumbuiza na  kuwafanya  watazamaji  kupata burudani ya kutosha





 

Post a Comment

Previous Post Next Post