Mwaka Mmoja Wa Rais Samia Waleta Neema Kigamboni

 Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imefanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa maji wa Kigamboni (Kisarawe II ) ili kujionea Maendeleo ya mradi huo ikiwa ni mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassani.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt.Christina Ishengoma amesema anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga pesa kwenye mradi wa maji wa Kisarawe II ili kuondoa hadha ya upatikanaji wa maji katika eneo la Kigamboni pamoja na maeneo ya pembezoni.

Pia ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kwa kuweza kusimamia na kutekeleza miradi huo maji kikamilifu.

"Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji tumeyapokea taarifa ya mradi wa Kisarawe II na pia tumetembelea ili kujiridhisha na kuona kuwa hakuna tatizo la kutaa mradi wa maji kwani wa DAWASA kwani kazi inaonekana" alisema Dkt. Ishengoma

Naye Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuongeza bajeti ya mwaka 2021/2022 kwenye Wizara ya Maji ili kuhakikisha wananchi wa Dar es Salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla wanapata majisafi na Salama ikiwa na lengo la kumtua mama ndoo kichwani.

"Mamlaka za maji nchini zinatekeleza miradi kama hii ya DAWASA ili kuweza kuondokana na tatizo la maji katika Mikoa yote hapa nchini" alisema Mahundi

Naye Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi wa Maji Kisarawe II unahusisha uendelezaji wa visima kumi na mbili vya maji vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 57 pamoja na ujenzi wa tanki la kuhufadhia maji litakaloweza kuhifadhi maji lita Milioni 15.

“Mradi huu unatekelezwa kwa sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ujenzi wa kituo cha kusukuma maji, kituo cha kupokea Maji, ulazaji wa mabomba ya maji na ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhi maji la lita milioni kumi na tano linalojengwa Kigamboni na awamu ya pili ikihusisha kazi ya kufunga njia za umeme kwenye visima na kutoa maji kwenye visima na kupeleka kwenye kituo cha kusukuma maji amesema Luhemeja.

Luhemeja  amesema Mradi huu ulianza kutekelezwa mwezi Disemba mwaka 2019 huku ukigharimu kiasi cha bilioni 24 fedha za ndani za Mamlaka na kukamilika kwakwe kutanufaisha wakazi 250,000 wa maeneo ya Kibada, Mjimwema, Masonga, Kimbiji, Mpera na maeneo ya karibu.
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu moja ya kisima chenye urefu mita 600 kwenda chini kilichopo katika kata ya Kisarawe II katika Wilaya ya Kigamboni wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea mradi huo Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu namna mabomba ya maji yatakavyolazwa mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa tanki la kuhufadhia maji linalojengwa Kigamboni wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea mradi huo Kigamboni mkoani Dar es Salaam

Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya aMajisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu ujenzi wa tanki la kuhufadhia maji litakaloweza kuhifadhi maji lita Milioni 15 linalojengwa Kigamboni wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea mradi huo Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi wakitembelea Mradi wa ujenzi wa Tanki la kuhifadhia maji wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea mradi huo Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Ziara ikiendelea
Picha ya Pamoja

Post a Comment

Previous Post Next Post