KAMISHNA MKUU TRA AKUTANA NA TAASISI ZINAZOFANYA KAZI KWA PAMOJA MPAKA WA NAMANGA

 Mwandishi Wetu

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Yusuph Juma Mwenda amekutana na taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa pamoja katika Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Namanga kilichopo mkoani Arusha kwa lengo la kusikiliza kero zao ili ziweze kutatuliwa na kuwezesha urahisi wa ufanyaji wa biashara mpakani hapo na kuongeza mapato ya serikali.

Akiongea na watumishi wa taasisi mpakani hapo, Kamishna Mwenda amesema kwamba, lengo la ziara yake mpakani hapo ni kuwatembelea na kusikiliza kero zinazowakabili ili kuweza kuzitatua na kurahisisha biashara mpakani hapo.

“Nmekuja kuwasikiliza na kuona changamoto mlizonazo na tuone namna gani tunaweza kufanya nini ili hii OSBP itumike kurahisisha shughuli za biashara kwa sababu biashara zikiwepo ndizo zinaleta makusanyo ya kodi na kuweza kuleta maendeleo ya nchi”, alisema Kamishna Mwenda.

Ameongeza kuwa, Serikali inazithamini taasisi zote zilizopo mipakani na TRA pia itaendelea kuonesha ushirikiano kwa taasisi nyingine za Serikali ili suala la utendaji kazi mpakani hapo linakua zuri katika kurahisisha biashara.

Aidha, amezishukuru taasisi zote za serikali zinazoonesha ushirikiano wa pamoja katika kuhudumia wasafiri na wasafirishaji mpakani hapo na ameahidi kuendelea kushirikiana na taasisi hizo na amesisitiza kuwa, taasisi hizo hazinabudi kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za mpakani.

Kwa upande wao wawakilishi wa taasisi zilizohudhuria mkutano huo zimempongeza Kamishna Mkuu wa TRA kwa kuwatembelea na kusikiliza changamoto zao na wameahidi kutoa ushirikiano ili biashara mpakani hapo iwe rahisi. 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda akiongea na watumishi wa taasisi mbalimbali katika Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Namanga mkoani Arusha wakati alipotembelea na kuongea na watumishi wa taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa pamoja mpakani hapo tarehe 10 Julai, 2024.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda akipata maelezo kuhusu utendaji kazi wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Namanga mkoani Arusha wakati alipotembelea na kuongea na watumishi wa taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa pamoja mpakani hapo tarehe 10 Julai, 2024
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda akipata maelezo kuhusu utendaji kazi wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Namanga mkoani Arusha wakati alipotembelea na kuongea na watumishi wa taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa pamoja mpakani hapo tarehe 10 Julai, 2024











Post a Comment

Previous Post Next Post