MALIASILI NA UTALII YAANZA KUTEKELEZA MPANGO WA MIAKA 10 YA KUMUENZI MWL NYERERE

 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Francis Michael akifunfua kikao kazi cha wataalam wa Wizara ya Maliasili na wadau mbalimbali kuweka mikakati ya utekelezaji wa adhimisho la miaka 100 ya Mwl Nyerere (Mwl@100) Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza na wanahabari juu ya maadalizi ya maadhimisho ya miaka 100 ya Mwl Nyerere (Mwl@100) Jijini Dodoma.

Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Francis Michael na wajumbe wengine wakifuatilia uwasilishaji wa maandalizi ya maadhimisho ya miaka 100 ya Mwl Nyerere (Mwl@100) Jijini Dodoma.

Mfano wa namna uwanja wa tukilo la maadhimisho ya miaka 100 ya Mwl Nyerere (Mwl@100) Jijini Dodoma.

…………………………

Na Sixmund J. Begashe

Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka kumi wa  Kuenzi na Kusherehekea Urithi wa Utamaduni unaotokana na Maisha ya Hayati Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyarere.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Francis Michael wakati akifungua kikao kazi cha wataalam wa Wizara ya Maliasili na wadau mbalimbali kuweka mikakati ya utekelezaji wa adhimisho la miaka 100 ya Mwl Nyerere (Mwl@100) Jijini Dodoma.

Dkt. Michael aliongeza kuwa lengo la Wizara ni kuhakikisha urithi unaotokana na maisha ya Baba wa Taifa unatumika katika kuliunganisha Taifa kijamii, kisiasa na kiuchumi hivyo ameziagiza Taasisi zote za Wizara kushiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Aprili13, 2022, Butiama Mkoa wa Mara.

Tangu kuzaliwa kwake, Mwalimu alionesha uzalendo kwa nchi yake na kujitoa katika harakati mbalimbali za mapambano ya kudai uhuru na kujenga uchumi sio wa Taifa lake tu bali kokote kule kulikokuwa na uonevu”. Amesisitiza Dkt. Michael

Hata hivyo Dkt Michael ameeleza kuwa jambo la muhimu ni kuhakikisha fursa hii inatumika kutangaza utalii  pamoja na kuonesha mchango wa Mwalimu Nyerere katika sekta hiyo na kutaka Bodi ya Utalii Tanzania na Taasisi za Wizara zishiriki ipasavyo kutangaza Adhimisho hilo.  

Akielezea maandalizi ya adhimisho hilo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale nchini Dkt. Kristowaja Ntandu ameleza kuwa hadi sasa Taasisi na wadau zaidi ya 10 zimejitokeza kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katka maadhimisho hayo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga ametaja matukio yatakayo pamba maadhimisho hayo kuwa ni pamoja na matembezi, mchezo wa bao, burudani mbalimbali za muziki wa dansi, ngoma za asili, kughani mashairi, maonesho ya Wizara na Taasisi mbalimbali.

Maadhimisho haya pia yataambatana na hafla ya kifamilia itakayofanywa na ukoo wa Mwalimu Nyerere ikihusisha ibada kanisani, midahalo, makongamano na Semina, Onesho maalum la mchango wa Mwalimu Nyerere katika maendeleo ya nchi pamoja na Kalamu ya Mwalimu”. Aliongeza Dkt Lwoga

Adhimisho hilo ni sehemu ya Mpango wa miaka 10 wa Kuenzi na Kusherehekea Urithi wa Utamaduni unaotokana na Maisha ya Mwalimu Julius Nyarere ambao kwa nyakati mbalimbali litakuwa likiadhimishwa kila mwaka Aprili 13 na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Post a Comment

Previous Post Next Post