Mhe. Mchengerwa awataka watendaji kuchapa kazi

 Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka Watendaji wote wa Wizara yake kujitafakari utendaji wao na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuendelea kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. 

Mhe. Mchengerwa ameyasema haya wakati alipokuwa akifungua kikao cha kupitishwa kuhusu maandalizi ya Bajeti na Randama kwa mwaka wa fedha 2022/23 na kamati ya bajeti leo Machi 20, 2022 katika ukumbi wa MAELEZO jijini Dodoma.

"Naomba niwatake watendaji wote kufanya kazi kwa kufuata maadili na taratibu za kazi za Serikali ili kuleta  mafanikio  kwa wananchi kwa ujumla". Amefafanua Mhe. Mchengerwa

Aidha, amewataka Wakuu wa Idara wote kuwa na vikao vya kiutendaji na watumishi wao ili kuleta mageuzi  ya kiutendaji.

Pia amewataka watendaji kufanya kazi kama timu  mmoja huku wakifungua milango ya wadau  kama wasanii ili  kujua  haki zao. 

“Watendaji tokeni waelezeni wasanii ili waweze  kujisajili ili waweze  kupata  haki zao na wapate  manufaa”. Amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Kwa upande mwingine, Mhe. Mchengerwa amesema Wizara imefanya mambo makubwa kwenye sekta za michezo, sanaa na Utamaduni na kwamba kinachotakiwa sasa ni kuendelea kufanya vizuri. 

Aidha, ametumia tukio hilo kumshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kusaidia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali yake.






Post a Comment

Previous Post Next Post