WAZIRI JAFO AAHIDI ATAHAKIKISHA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZILIZOSALIA ZINAPATIWA UFUMBUZI

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Said Jafo na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Hamad Hassan Chande wakiwasili katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino leo Aprili mosi, 2021.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (kushoto) akiwaongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Said Jafo na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Hamad Hassan Chande kuelekea katika ofisi zao mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino leo Aprili mosi, 2021.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Said Jafo akizungumza na Menejimenti ya Ofisi hiyo na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) baada ya kuwasili katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino leo Aprili mosi, 2021.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Hassan Chande akitoa neno la shukrani mara baada ya baada ya kuwasili katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba jijini Dodoma na Waziri Selemani Jafo mara baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino leo Aprili mosi, 2021.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) akizungumza wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Said Jafo na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Hamad Hassan Chande mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Chamwino leo Aprili mosi, 2021.

Sehemu ya Menejiemnti ya Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa wamejipanga kuwasubiri mawaziri wa Ofisi hiyo walioapishwa Ikulu jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

************************************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Said Jafo amesema atahakikisha changamoto za Muungano zilisosalia zinapatiwa ufumbuzi.

Ameyasema hayo hii leo mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Makamu wa Rais na kukutana na Menejimenti ya Ofisi yake na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini.

“Nashukuru kwa mapokezi mazuri, ila tuchape kazi tunahitaji kupata matokeo chanya kwa kazi tunazo simamia yaani Muungano na Mazingira” Jafo alisisitiza.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Hamad Chande amesisitiza ushirikiano baina ya watumishi katika kuhakikisha malengo ya kudumisha Muungano na kusimamia Mazingira yanatekelezeka.

Akiwasilisha taarifa ya Ofisi yake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo amewahakikishia ushirikiano Mawaziri na kuwakaribisha kwa niaba ya watumishi 

Post a Comment

Previous Post Next Post