MAAFISA TRA WAWATEMBELEA WALIPA KODI WA MTWARA

 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kodi Mtwara, Maimuna Khatib akifurahia jambo na Hamza Hakika Katani mfanyabiashara wa Pembejeo na Pikipiki Wilayani Masasi mkoa wa Mtwara, alipokua katika ziara ya kuwatembelea wafanyabiashara wilayani hapo kwa lengo la kuwashukuru kwa kulipokodi kwa hiyari na kusikiliza changamoto leo Dèsemba 16.2024




MENEJA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kodi Mtwara, Maimuna Khatib leo Desemba 16, 2024 ameongoza timu ya maofisa wa kodi kutoka TRA Dar es Salaam kuwatembelea walipakodi wa Masasi kwa lengo la kuwashukuru kwa kulipa kodi kwa hiyari sambamba na kuwasikiliza changamoto zao kwa lengo la kuzitatua.

Maimuna amesema hatua hiyo inakuja ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Kamishna Mkuu la kuwashukuru na kuwasikiliza walipakodi.

Aidha, Maimuna ametumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha walipakodi kufanya malipo ya kodi zao awamu ya nne mapema kabla ya tarehe 31 ya mwezi huu wa Desemba ili kuepusha usumbufu.

Post a Comment

Previous Post Next Post