WAZIRI CHAMURIHO ATAKA USHIRIKIANO

 

Katibu Mkuu-Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa utangulizi, katika kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri mpya wa Wizara hiyo, Mhe. Mwita Waitara, kilichofanyika katika ofisi za Wizara hiyo Mtumba, jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu-Uchukuzi,  Gabrieli Migire, akifafanua jambo katika kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri mpya wa Wizara hiyo, Mhe. Mwita Waitara, kilichofanyika katika ofisi za Wizara hiyo Mtumba, jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akifafanua jambo wakati wa kikao na Menejimenti ya Wizara cha kumtambulisha Naibu Waziri Mpya wa wizara hiyo, Mhe. Mwita Waitara (kushoto) kilichofanyika Mtumba, jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya, akifafanua jambo katika kikao cha Menejimenti ya Wizara cha kumtambulisha Naibu Waziri mpya wa Wizara hiyo, Mhe. Mwita Waitara (wa kwanza kushoto), kilichofanyika katika ofisi za wizara hiyo mtumba, jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara, akizungumza katika kikao chake cha kwanza na Menejimneti ya wizara hiyo, mara baada ya kuapishwa 1 aprili 2021. Kikao hicho kilifanyika katika ofisi za wizara hiyo Mtumba, jijini Dodom

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho (kulia) akimkabidhi kadi Naibu Waziri Mpya wa Wizara hiyo, Mhe. Mwita Waitara , ikiwa ni ishara ya kumkaribisha mara baada Naibu Waziri huyo kutambulishwa kwa Menejimenti ya Wizara katika ofisi za Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, wakiwa katika kikao cha kwanza na kumkaribisha Naibu Waziri mpya Mhe. Mwita Waitara (hayupo pichani), kilichofanyika katika ofisi za wizara, Mtumba, jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………………..

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho ameitaka Menejimenti ya Wizara kutoa ushirikiano kwa Naibu Mawaziri wa wizara ili kutimiza dhamira ya Serikali  ya kukamilisha miradi kwa wakati na ubora.

Akizungumza wakati wa kikao cha kumkaribisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Mwita Mwaitara, Waziri Chamuriho amesisitiza umuhimu wa utoaji wa taarifa kwa wakati na kusisitiza uratibu mzuri wa utoaji wa taarifa hizo ili kuepuka mgongano.

“Mafanikio ya Wizara kwa sehemu kubwa yanategemewa na ushirikiano utakaooneshwa kuanzia kwenye usimamizi wa miradi mikubwa ya kimkakati na uratibu wa taarifa zinazotolewa kuanzia kwenye menejimenti na taasisi’ Amesema Waziri Chamuriho.

Waziri Chamuriho amesema Wizara imebeba miradi mikubwa ya nchi, ikiwemo reli, ndege, meli, vivuko, madaraja na barabara hivyo ni muhimu kwa Manaibu hao kujipanga kukagua miradi ya maendeleo kwa kushirikiana ili kubaini changamoto na kuzitafutia utatuzi wa haraka.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Godfrey Kasekenya amesema ushirikiano uliopo kati yake na Menejimenti umemfanya afanye kazi kwa weledi na kuifahamu sekta kwa haraka.

“Toka nimeteuliwa kuwa Naibu Waziri niseme ukweli nimepata ushirikiano mkubwa sana kutoka kwa menejimenti wakati wote nilipokuwa nikihitaji taarifa yoyote niliipata kwa wakati na kupewa maelezo ya kina” amesema Naibu Waziri Kasekenya.

Naye Naibu Waziri Waitara ameomba kupata ushirikiano kwa kupewa taarifa za maendeleo ya miradi ya maendeleo kwa wakati ili kuweza kufanya kazi yenye matokeo chanya kwenye sekta mpya aliyoteuliwa.

Aidha, Katibu Mkuu- Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, amesema kuongezewa kiongozi kutaongeza chachu ya kuwajibika katika usimamizi na kuahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi wote  kwa wakati.

Mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu, 31 Machi, 2021 yameongeza Idadi ya Manaibu Waziri kutoka mmoja na kuwa wawili ili kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi.

Imetolewa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Post a Comment

Previous Post Next Post