RC DANIEL CHONGOLO AIPONGEZA TRA KWA KAZI NZURI YA UKUSANYAJI MAPATO

 Na Mwandishi Wetu,

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, leo tarehe 19 Disemba 2024, ametembelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Ndositwe Haonga, ofisini kwake. Ziara hii ni sehemu ya kampeni ya kitaifa inayolenga kuwashukuru walipakodi kwa mchango wao mkubwa katika mapato ya serikali.

Katika kampeni hii, walipakodi wa makundi mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara wakubwa, wa kati, na wadogo, wanapewa shukrani kwa njia ya zawadi. Hatua hii inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya TRA na wadau wake, wakiwemo viongozi wa dini, viongozi wa serikali na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, katika juhudi za kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unafanikiwa.

Mhe. Chongolo amepongeza hatua ya TRA kuwakumbuka na kuwashukuru wateja wao wakubwa, akisema ni kitendo cha kuimarisha uhusiano wa karibu, jambo ambalo linasaidia kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya ukusanyaji wa mapato.

Aidha, Mhe. Chongolo ametoa Pongezi kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni Bw. Yusuph Mwenda. akimpongeza kwa kazi nzuri ambayo imekuwa ikiendelea kufanyika kwa ufanisi mkubwa.


Post a Comment

Previous Post Next Post