WAZIRI KALEMANI BEI YA KUWAUNGANISHIA UMEME WANANCHI WA DODOMA NI SH.27,00 TU

 

Afisa Mtendaji Kata ya Ntyuka Bi.Christina Mpete,akitoa taarifa kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme katika baadhi ya maeneo ya mitaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwemo iliyopo katika Kata ya Ntyuka iliyofanyika Aprili 01, 2021.

 

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme katika baadhi ya maeneo ya mitaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwemo iliyopo katika Kata ya Ntyuka iliyofanyika Aprili 01, 2021.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na Mkazi wa Kata ya Ntyuka wakati wa  ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme katika baadhi ya maeneo ya mitaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwemo iliyopo katika Kata ya Ntyuka iliyofanyika Aprili 01, 2021.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,akiwaonyesha kitu wakati wa  ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme katika baadhi ya maeneo ya mitaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwemo iliyopo katika Kata ya Ntyuka iliyofanyika Aprili 01, 2021

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme katika baadhi ya maeneo ya mitaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwemo iliyopo katika Kata ya Ntyuka iliyofanyika Aprili 01, 2021

Mbunge ya Jimbo la Dodoma Antony Mavunde,akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,ambaye alifanya ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme katika baadhi ya maeneo ya mitaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwemo iliyopo katika Kata ya Ntyuka iliyofanyika Aprili 01, 2021

……………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa, kuanzia leo maeneo yote ya Mkoa wa Dodoma yataunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi ya 27,000 tu na si zaidi ya hapo.

Dkt. Kalemani amesema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme katika baadhi ya maeneo ya mitaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwemo iliyopo katika Kata ya Ntyuka iliyofanyika Aprili 01, 2021.

Amesema kuwa katika maeneo yote yenye sifa za vijiji ambayo yapo katika jiji wananchi wataunganishiwa umeme kwa gharama ya Sh. 27,000 na siyo vinginevyo.

“Na hapa lazima niweke msisitizo kiasi cha kulipia mwananchi ni Sh. 27,000 na siyo vingine na kwa wale waliolipia kiasi cha juu mtawarudishia katika bili zao za umeme”amesema Dk. Kalemani

Aidha Dk.Kalemani amewataka wananchi wote ambao wametandaza nyaya katika nyumba zao kulipia gharama hizo haraka iwezekanavyo ili kuunganishiwa umeme.

Ameagiza kuwa, transfoma ziongezwe kwenye maeneo mbalimbali nchini kwani inapofungwa transfoma moja katika eneo lenye makazi mengi, inapelekea umeme kukatika mara kwa mara.

Hata hivyo Dk.Kalemani,amesema kuwa Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya ambao wameshidwa kuwaunganishia umeme wananchi waliolipia kwa wakati pamoja na wale walioshidwa kudhibiti kukatika kwa umeme bila sababu ndani ya siku 14,kuanzia leo   wataondolewa katika nafasi zao.

“Januri 15,mwaka huu niliwapa muda wa miezi mitatu mameja wote wa Tanesco kuwa wamemaliza zoezi la kuwaunganishia umeme wananchi waliolipia na hadi leo zimebaki siku 14, hivyo wale wote watakaoshindwa wajiandae kufungasha vilago vyao”amesema Dk. Kalemani

Dk.Kalemani amesema kuwa mara baada ya siku hizi kuisha tutaonana wabaya kwani walioshindwa kutekeleza agizo hili watabidi watupishe kwani wameshindwa kuzifanyia kazi nafasi zao tutawavua nyazifa zao.

Aidha, amesema  kuwa pia kwa Mameneja, ambao wameshindwa kudhibiti matukio ya kukatia kwa umeme katika maeneo yao watawajibika.

Naye Mbunge ya Jimbo la Dodoma Antony Mavunde, amesema kuwa anaishukuru serikali kwa niaba ya wakazi wa mkoa wa Dodoma kwa kuwafikishia huduma hiyo ya umeme.

“Mhe. Waziri tunashukuru sana kwa kutusogeza huduma hii na mimi pamoja na viongozi wa eneo hili tutaendelea kuhamasisha wananchi kulipia na kupata umeme kama ilivyo azma ya serikali yetu chini ya Rais Samia Suluhu Hassan”amesema

Post a Comment

Previous Post Next Post