TIC YAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUWEKEZA TANZANIA

  Meneja wa Kanda ya Mashariki TIC, Bw.Bevin Ngezi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mradi wa Mlimani City na kufanya mazungumza na uongozi wa Mlimani Holdings Limited (Mlimani City) leo Jijini Dar es Salaam.   Mkurugenzi Mkuu wa Mlimani Holdings Limited (Mlimani City) Bw.Pastory Mrosso akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelewa na Meneja wa Kanda ya Mashariki TIC leo kwenye ofisi yake Jijini Dar es Salaam.  Meneja wa Kanda ya Mashariki TIC, Bw.Bevin Ngezi (katikati) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mlimani Holdings Limited (Mlimani City) Bw.Pastory Mrosso mara baada ya kutembelea mradi huo leo Jijini Dar es Salaam.  Meneja wa Kanda ya Mashariki TIC, Bw.Bevin Ngezi (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mlimani Holdings Limited (Mlimani City) Bw.Pastory Mrosso mara baada ya kutembelea ofisi za mradi huo leo Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Bevin Ngenzi akiwa na ujumbe kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania wakiwa katika picha na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mlimani Holdings Ltd, Bw. Pastory Mrosso ambao ni wawekezaji wa mradi wa Mliamani city baada ya kikao na ukaguzi wa mradi huo, leo Aprili 22, 2021 Dar es Salaam.

******************************

NA EMMANUEL MBATILO

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimewakaribisha wawekezaji kuendelea kuwekeza hapa nchini kwani nchi ipo salama na Serikali ipo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kupata mafanikio.

Ameyasema hayo leo Meneja wa Kanda ya Mashariki TIC, Bw.Bevin Ngezi alipotembelea Mlimani City na kukutana na muwekezaji wa mradi huo.

Akizungumza baada ya kukutana na muwekezaji wa Mlimani Holdings limited (Mlimani City), Bw.Ngezi amesema Tanzania ipo tulivu kisiasa na ina mafanikio makubwa kibiashara ambapo ni rahisi sana muwekezaji kuwekeza na kuweza kupata mafanikio makubwa.

“Tumeona Mlimani holdings limited wameweza kuwekeza na kupata mafanikio hivyo tunawatia moyo wawekezaji wazawa na wawekezaji wengine kuja kuwekeza Tanzania kwa maana Tanzania kuna watu wema na kwenye mafanikio ha kibiashara”. Amesema Bw.Ngezi.

Aidha Bw.Ngezi amesema kuwa uwekezaji uliofanywa na Mlimani Holdings Limited umesaidia kutoa ajira kwa watanzania pamoja na kuinua maisha ya watanzania kwa ujumla.

“Uwekazaji Uliofanywa na Mlimani Holdings Limited umesaidia kutoa ajira zaidi ya elfu 2 kwa watanzania pia wapo wanaokuja kufanya biashara na kutoa kwahiyo wapo wengi wamefaidika na uwepo wa Mlimani City”. Amesema Bw.Ngezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mlimani Holdings Limited (Mlimani City) Bw.Pastory Mrosso amesema tangu kuanzishwa kwa mradi huo, TIC imekuwa nyuma ya mafanikio ya Mlimani City mpaka ulipofikia kwa maana serikali ilikuwa na sehemu ya utekelezaji wa mradi huo.

“Serikali imejitahidi kwa kila hali kuhakikisha mradi unatekeleza kwa yale yote muwekezaji aliyokuwa amekusudia na kuleta manufaa makubwa kwa watanzania”. Amesema Bw.Mrosso.

Pamoja na hayo Bw.Mrosso amesema serikali inapata mapato kupitia kodi kutoka kwa muwekezaji pamoja na waliowekeza maduka kwenye mradi 

Post a Comment

Previous Post Next Post