WAZIRI JAFO AKUTANA NA UONGOZI WA VODACOM TANZANIA FOUNDATION

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo leo tarehe 22/4/2021 amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Vodacom Tanzania Foundation wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano Bi. Rosalynn Mworia. Pamoja na mambo mengine Vodacom Tanzania wameelezea program za Mazingira walizopanga kutekeleza. Waziri Jafo amewaahidi ushirikiano wa karibu katika kuendeleza agenda ya Uhifadhi wa Mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Vodacom Tanzania Foundation mara baada ya kufanya mazungumzo hii leo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba Dodoma. Kulia ni Bi. Rosalynn Mworia Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano na Bi. Sandra Oswald Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation

Post a Comment

Previous Post Next Post