DR JAFO ASISITIZA UMOJA UPENDO MSHIKAMANO KWA MAENDELEO YA TAIFA

 

NA MWANDISHI WETU

Katika kufikia maendeleo endelevu kwa jamii bila ya umoja, upendo na mshikamano haiwezi kabisa jamii Kupata Mafanikio wanayoyataka akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika Mafunzo kwa Viongozi wa kata wa Chama na jumuia zake wilaya kisarawe jana minaki 31.12.2022,
Katika Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Jumuia ya wanawake Mkoa wa pwani Mhe Zainab vulu alisisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika jamii,
*”Naomba kuwaambiwa umoja wetu sisi Wana CCM Ni Lulu hivyo tuutunze na kuuwenzi ili tupate Mafanikio Zaidi alisikika mhe Vulu”*
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya kisarawe Comred Halfani Sika Alisisitiza mshikamano miongoni mwa wanachama Pamoja na Kusisitiza maendeleo ya Jamii kwa Kufanya Kazi na kuacha majungu miongoni mwa wanachama ndani ya kisarawe,
*”Hivi sasa kumekua na badhii ya wanachama badala ya Kufanya Kazi kwa maendeleo wao wanahubiri majungu hatuendi hivyo sisi kisarawe kabisa alisisitiza Komdred Sika*
Nae Mbunge wa Jimbo la kisarawe mhe Dr Selemani Jafo alisisitiza umoja upendo na Mshikamano miongoni mwa wana kisarawe na taifa kwa ujumla Kama ambavyo Mwenyekiti wa Chama taifa anavyosisitiza kwa watanzania Wote,
*”Leo hi Hapa tumewasilisha Tarifa ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii zetu huko Kata zetu zote kumi na Saba za kisarawe shime hiyo miradi tuitunze kwa maslah ya taifa Kama mhe RAIS SAMIA alivyotutuma sisi Wasaidizi wake kwenu alisisitiza Dr JAFO”
Uwasilishaji wa Tarifa ya miradi kwa Wajumbe ulifanywa na Mbunge mwenyewe kwa kufafanua miradi katika Elimu,Afya, Miundombinu ya Barabara,Kilimo,ufugaji,Mikopo na Umeme, Kutoka 2020-2022

Post a Comment

Previous Post Next Post