NAIBU WAZIRI WA NISHATI AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA

 

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato ( Mb.) akizungumza na viongozi wa Idara na Taasisi tajwa hapo juu.( hawamo picha)

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato (Mb.) leo amekutana na viongozi wa Idara ya Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati pamoja na Uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja ( PBPA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji ( EWURA) katika kikao cha kiutendaji kuhusiana na Sekta ya Petroli na Gesi kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Viongozi mbalimbali wa Idara ya Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati, viongozi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja ( PBPA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji ( EWURA), wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa na Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati  Eng. Marwa Petro ( hayumo pichani) wakati wa kikao hicho kilichofanyika leo kwenye ofisi za Wizara ya Nishati, zilizopo Mtumba jijini Dodoma.  

Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati Eng. Marwa Petro, ( kushoto kwa Naibu Waziri Byabato) akiwasilisha mada wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato ( Mb.) na viongozi wa Idara ya Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati pamoja na Uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja ( PBPA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA) katika kikao cha kiutendaji kuhusiana na Sekta ya Petroli na Gesi kilichofanyika leo kwenye ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mtumba , jijini Dodoma.

Post a Comment

Previous Post Next Post