WATAALAM WA KUCHOMA NYAMA YA NYANI, WAHUNZI WAKUTANA NA DC KARATU JIOPAKI YA NGORONGORO LENGAI.

Na Mwandishi wetu Eyasi,

Kamati  ya Usalama ya Wilaya ya Karatu, ikiongozwa na  Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.  Dkt. Lameck Karanga, imekutana na baadhi ya wananchi wa kabila la wahadzabe, kabila ambalo kwao nyama ya nyani ni kipaumbele kikubwa katika maisha yao na kukutana na wadatoga wanaojihusisha na  uhunzi ,ziara ambayo imefanyika katika eneo la Eyasi wilayani humo.

Kabila la wahadzabe ambalo linaheshimika kutokana na mila na silka zake za kiasili linaamini kuwa nyama ya nyani ndiyo nyama bora na tamu kuliko zote duniani na limekuwa likimtumia mnyama huyo kama kielelezo muhimu kwa maisha yao huku kabila la wadatoga wakiendelea kutumia zana za kale katika uhunzi wa kufua bidhaa mbalimbali za kitamaduni.

Makabila yote mawili yanapatikana ndani ya jiopaki ya Ngorongoro Lengai inayopatikana wilaya ya  Karatu,  Ngorongoro na Monduli ,wilaya ambazo baadhi ya maeneo yake yanaunda jiopaki ya kidunia inayojulikana kama  Ngorongoro Lengai  Global Geopark  inayotambuliwa na Shirika la Sayansi,Elimu na Utamaduni ( UNESCO).

Akizungumza na jamii ya makabila hayo  Dkt. Lameck Karanga amewapongeza wananchi hao kwa kuendelea kutumisha mila na tamaduni za asili huku wakiwa kielelezo katika utunzaji wa amani na utulivu katika maeneo yao na kuwataka kuendelea kuwa kielelezo bora cha jamii nchini kwani serikali itaendelea kuwalinda na kuboresha shughuli za utalii katika eneo hilo.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro  bwana  Joas Makwati  ameeleza kuwa mradi wa Jiopaki ya Ngorongoro unanufaisha jamii zinazokaa ndani na nje ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuwa  Shughuli za  ufugaji, uwindaji na  kilimo hutegemea uwepo wa maji uhifadhi wa misitiu ya Ngorongoro. 

Kabila la wahadzabe linaloishi pembezoni mwa eneo la Eyasi limekuwa likisifika kutokana na utaalam wake wa kuchoma na kula nyama za nyani jambo ambalo limewafanya wageni kutoka ndani nan je ya nchi kuwatembelea ili kuona jinsi mnyama huyo alivyokuwa tunu kwa kabila hilo.

Nyama ya nyani iliyochomwa vizuri kwa mujibu wa kabila hilo ina vionjo vitamu kutokana na mnyama huyo kula mizizi,matunda na mimea pori ambayo huifanya nyama yake kuwa  na ladha ya kuvutia na yenye kuufanya mwili uweze kuhimili magonjwa mbalimbali.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post