TTB YAKUTANA NA WATAYARISHAJI WA KIPINDI CHA AZAM TV CHA VIUMBE HAI

  Mkurugenzi wa Masoko wa TTB, Bi. Mindi Kasiga akisikiliza kwa makini ujumbe unaotolewa na Bw. Mani Bakhresa wa Televisheni ya Azam wakati wa mkutano.

Wajumbe wa mkutano wa TTB na Televisheini ya Azam wakiwa katika picha ya pamoja

Baadhi ya wafanyakazi wa TTB na Televisheni ya Azam wakiwa katika mazungumzo.

Mkurugenzi wa Masoko wa TTB, Bi Mindi Kasiga akisisitiza jambo mara baadaya ya kumaliza mkutano.

*************************************

 
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) leo tarehe 21/8/2020 imekutana na waandaaji wa kipindi cha televisheni kijulikanacho kama “Viumbe Hai” kinachorushwa na Azam TV kwa lengo la kupanga mikakati ya kushirikiana katika kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.
 
Kipindi hicho kinachorushwa mara nne kwa wiki, kwa msimu (Season), kimejikita zaidi katika kuelimisha umma kuhusu tabia za wanyama mbalimbali wanaopatikana katika vivutio vya utalii vya Tanzania. 
 
Akiongea wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za TTB jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masoko TTB, Bi Mindi Kasiga alisema “ushirikiano baina ya TTB na Azam ni wa kimkakati kwa kuwa kwa pamoja tunatoa elimu kwa umma kuhusu utalii wa wanyama na viumbe hai.
Viumbe Hai inatoa hamasa kwa watazamaji kujionea wanyama wakiwa katika maisha yao halisi na kusababisha idadi ya watalii wa ndani na nje kuongezeka”.
 
Mwongozaji wa kipindi hicho Bw. Mani Bakhresa alisema Viumbe Hai kina watazamaji zaidi ya milioni tatu ndani na nje ya nchi na kuongeza kuwa ushirikiano na TTB umewezesha utayarishwaji wa Msimu wa Nne wa
kipindi hicho kusheheni vivutio ambavyo Watanzania wengi hawajawahi kuviona.

“Watazamaji wetu wajiandae na msimu huu kuona tabia za Nyumbu wakivuka mto, Flamingo wa Ziwa Natron na Mbwa mwitu adimu sana kuonekana” alisema Bw. Bakhresa. 

Msimu wa Nne wa Viumbe Hai unatarajiwa kuanza kuruka hewani pindi baada ya kukamilika utayarishwaji wa vipindi (episodes) vyote 12 vitakavyokamilisha Msimu huo. 

Ili kuhamasisha na kutangaza utalii wa ndani, Bodi ya Utalii inakaribisha vyombo vingine vya habari kuibua vipindi kama ‘Viumbe Hai’ vitakavyotoa hamasa kwa umma na kujenga utamaduni wa kutalii na kutembelea vivutio
vya utalii vya Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post