JKCI yapokea msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram –ECG

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) kutoka kwa Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Thamani ya mashine hiyo ni milioni 17.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpulizia kisafisha mikono (hand sanitizer ) Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) mara baada ya kumkabidhi msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Thamani ya mashine hiyo ni milioni 17.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wazazi kuhusu umuhimu wa kufanya kipimo cha kuchunguza moyo wa mtoto aliyepo tumboni kwa wamama wajawazito (Fetal Cardiograph). Wazazi hao walifika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwaleta watoto wanaotibiwa Jkci kliniki.

Post a Comment

Previous Post Next Post