TBS WANDAA BONANZA LA MICHEZO ILI KUWAWEKA KARIBU WAFANYAKAZI WA SHIRIKA HILO.

  Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema akikagua vikosi vya mpira wa miguu katika bonanza linaloshindanisha wafanyakazi wa TBS, katika michezo mbalimbali.      

************************************

EMMANUEL MBATILO

Michezo pamoja na mazoezi ya viungo vya mwili kwa Wafanyakazi ni sehemu muhimu kwa maendeleo ya rasilimali watu, husaidia kuimarisha afya,maelewano na ushindani wa kirafiki wenye matokeo chanya.

Ameyasema hayo leo Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema katika bonanza linaloshindanisha wafanyakazi wa TBS, katika michezo mbalimbali.

Akizungumza katika Bonanza hilo linalokwenda kwa jina VIWANGO SPORTS BONANZA, Bw.Ndibalema amesema ubora katika michezo huongeza hisia ya mafanikio na uzalendo.

Aidha Bw.Ndibalema amesema dhumuni la bonanza hilo ni kukutanisha wafanyakazi wote wa TBS kupitia michezo.

“Tukishiriki katika bonanza tunaongeza wigo wa kufahamiana, kujenga undugu, kupunguza msongo wa mawazo pamoja na kuburudika”. Amesema Bw.Ndibalema.

Kwa upande wake Mhandisi wa Umeme,kitengo cha Uandaaji wa Viwango TBS, Bi.Neema Semwa amesema japo bonanza hilo limekuwa la kwanza kwao basi litakuwa endelevu kila mwaka na litaboreshwa zaidi ili kuleta hamasa kwa Watumishi kushiriki katika michezo.

Pamoja na hayo Bi.Neema amesema mazoezi ya viungo ni muhimu kwani unaweza kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza kama magonjwa ya moyo, kisukari na mengineyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post