NEC YAZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUTOCHANGANYA ELIMU YA MPIGA KURA NA KAMPENI

 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Mstaafu Mbarouk Mbarouk akifungua kikao cha Asasi za kiraia  zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa Uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba 28, Mwaka huu leo Jijini Dodoma.

 Meza Kuu wakifatilia mada mbali mbali zinazowasilishwa kwa asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.     Baadhi ya wawakilishi wa Asasi za Kiraia waliopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu walio hudhulia katika kikao 

……………………………………………………………..

Na. Majid Abdulkarim, Dodoma

Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imezitaka Asasi za Kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi Mkuu kutokutumia nafasi hizo kuchanganya elimu ya mpiga kura na kampeni za vyama vya siasa.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Mstaafu Mbarouk Mbarouk wakati akifungua kikao cha Asasi za kiraia  zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa Uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba 28, Mwaka huu.

Mbarouk amesema lengo ni kuzitaka asasi hizo  kuwa makini na mambo ambavyo yanaweza kuleta sintofahamu bila ya sababu yeyote ya msingi.

Aidha, Mbarouk amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa asasi yeyote itakayo bainika kukiuka maagizo na maelekeyo yaliyotolewa na Tume hiyo kuwa haitasita kusimamisha kibali chake wakati wowote.

“Wakati mwingine unaweza kudhani unatoa elimu ya mpiga kura, ambayo kimsingi haitakiwi kuegemea upande wowote na bila kujua ukajikuta unafanya kampeni, “ameeleza Mbarouk.

Mbarouk ameongeza kuwa inawezekana hilo likajitokeza kutokana na Mazingira wanayotolea elimu hiyo, kwa mfano kutumia jengo la Chama Cha siasa au eneo linalofahamika na watu kuwa ni la Chama Fulani.

Katika  hatua nyingine Mbarouk ameeleza kuwa maelekezo ya kutotuimia kwa ubia vibali walivyopewa na Tume  na asasi nyingine yoyote ile na hasa zile ambazo hazijapata vibali hivyo Tume inafahama kuwa baadhi ya asasi zilizopewa vibali wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, zilitumia vibali vyao kwa ubia na asasi nyingine.

“Kwa asasi ambazo zilibainika kufanya hivyo, imekuwa ni sababu moja wapo ya baadhi yao kukosa vibali kipindi cha uchaguzi wa mwaka huu,”amesisitiza Mbarouk.

Vile vile Mbarouk amesema kuwa  katika eneo la elimu ya mpiga kura Tume  haijaziachia asasi za kiraia na wadau wengine, unaendelea kutoa elimu ya mpiga kura kwa kutumia njia mbalimbali ili kuwafikia walengwa Kama vile, mikutano na wadau, tayari mikutani na wadau imeanza kuanzia Agost mosi mwaka huu.

Lakini pia Mbarouk amesema kuwa Tume inategemea kushiriki kwenye maonyesho mbalimbali ya kitaifa ambayo hukutanisha wadau, wapiga kura na wananchi kwa ujumla kwa mfano imeshiriki katika maonesho ya nanenane ya mwaka huu mkoni Morogoro na Dodoma, na itaendelea kufanya hivyo katika maonesho mengine.

Mbarouk amekumbushia kuwa Mambo muhimu ya kuzingatia katika utekelezaji wa kazi hiyo, kuwa ni pamoja na kuhakikisha kunakuwepo na mawasiliano na Tumee na wasimamizi vwa uchaguzi katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa kazi hiyo kwa mfano wanapotaka kubadilisha ratiba ili kurahisisha ufuatiliaj.

“kuhakikisha wanajitambulisha kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye Halmashauri wanazoenda kabla ya kuanza shughuli yoyote”amesisitiza Mbarouk.

Pia  kuhakikisha baada ya kukamilika kwa kazi hiyo wanaandaa taarifa na kuiwasilisha Tume kwa wakati.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Kumekucha Tanzania, Jovith Gaspar ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupatiwa elimu ili ifikapo Oktoba, 28 Mwaka huu waweze kujitokeza kwa wingi ili kuweza kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kuchagua kiongozi wanaomtaka kwa ajili ya maendeleo yao.

Post a Comment

Previous Post Next Post