
📍 Zanzibar
Wananchi na watalii waliotembelea Maonesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar yanayoendelea Fumba wameonesha kuvutiwa na fursa mbalimbali za uwekezaji zinazotolewa na Sekta ya Madini, hususan katika maeneo ya utafiti, uchimbaji mdogo, uchenjuaji, uongezaji thamani na biashara ya madini.
Wametembelea Banda la Tume ya Madini kujifunza taratibu za kujiandikisha, kuomba leseni za uchimbaji mdogo (PML), pamoja na kupata ushauri wa kitaalam kuhusu namna ya kushiriki kikamilifu katika sekta hiyo inayokua kwa kasi na kuchangia ajira, kipato na maendeleo ya uchumi wa nch