ELIMU YA KIDIJITALI YAPIGWA JEKI, SERIKALI NA HUAWEI WAAZIMIA USHIRIKIANO MPYA

 

Katika kuendeleza jitihada za Serikali za kuimarisha upatikanaji na ubora wa elimu katika ngazi zote nchini, Mhe. Wanu Hafidh, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Vincent Wen, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya Huawei.

‎Katika mazungumzo hayo pande zote mbili zimeazimia kuimarisha ushirikiano wa kuongeza matumizi ya teknolojia za kidijitali katika ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi mbalimbali za elimu. Sambamba na hilo wamekubaliana kushirikiana katika kukuza vipaji na kuimarisha miundombinu stahiki ya teknolojia ya Akili Unde (Artificial Intelligence).

‎Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu na Prof. Ladslaus Mnyone Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.

Post a Comment

Previous Post Next Post