NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Afya, Jenista Mhagama ameitaka Bodi ya 11 ya Ushauri ya Hospitali Binafsi kuhakikisha vituo vinavyoomba usajili vinakidhi vigezo vyote vya utoaji wa huduma bora za afya kabla yakupatiwa usajili pamoja na kufuatilia vituo vyote ambavyo vinatoa huduma bila usajili ili kupunguza malalamiko na changamoto kwa wananchi.
"Bodi hii pia, ina jukumu kubwa la kufanya ukaguzi wa vituo vya afya vilivyosajiliwa na kuhakikisha vinatoa huduma bora za afya kwa wananchi na kwa kuzingatia ngazi ambayo kituo hicho kimesajiliwa lakini vituo vinavyokiuka miongozo ya utoaji wa huduma iliyowekwa na Wizara mnatakiwa kuvichukulia hatua bila kuogopa lakini bila kuonea mtu.
"Sisi kama Serikali, tunao wataalamu. Tuna viongozi, wakaguzi na wasimamizi, wote kwa pamoja tufanye kazi kwa kusimamiana, na wote watakaotaka kuharibu mifumo yetu hao lazima tushughulike nao. Tumeshakubaliana kuwa Sekta Binafsi sio mshindani bali ni mshirika" Waziri Mhagama