Mwandishi Wetu,
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imewataka wakulima wa Jiji la Arusha na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi ili kusajiliwa kwenye mfumo wa mbolea za ruzuku na kupatiwa namba ya mkulima papo kwa papo.
Wito huo umetolewa na Afisa Udhibiti Ubora wa TFRA Kanda ya Kaskazini, Bi. Lydia Kalala, alipokuwa akihojiwa na Televisheni ya Taifa (TBC) katika viwanja vya Sheikh Abeid Amir, ndani ya banda la Wizara ya Kilimo.
Maonesho haya ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yatakayofikia kilele tarehe 8 Machi 2025.
Kalala ameongeza kuwa, mbali na kusajiliwa, wakulima pia watapewa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mbolea ili kuboresha uzalishaji wao na kuongeza usalama wa chakula.