MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ARIDHISHWA NA MABORESHO YA JENGO LA DAR ES SALAAM

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amezungumzia kuridhishwa kwake na maboresho ya Jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lililoko Kivukoni, Jijini Dar es Salaam. 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo wakati akizungumza na Kamati ya Wataalamu ya Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliokutana tarehe 5 Machi, 2025 katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kivukoni Jijini Dar es Salaam 

Aidha, Mhe. Johari amesema kuwa kutokana na umuhimu na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaona ipo haja Ofisi hizo za Dar es Salaam kuongekeza hadhi na kuwa Ofisi Kuu ndogo.

 “Ni Matarajio yangu kuwa Ofisi hii ibadilike kutoka kuwa Ofisi ya Mkoa na iwe Sub-head Office”.Alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa upande wake, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samwel M. Maneno alimshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika Ofisi hizo, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuzitunza ili ziendelee kuwa bora wakati wote. 

“Tunakushuru sana Mhe. Mwanasheria Mkuu kwa maboresho haya ambayo yameboresha muonekano wa Ofisi zetu, na sisi tutazitunza na kuzifanya ziendelee katika ubora huu.” Alisema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

       


Post a Comment

Previous Post Next Post