Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (kulia) Taarifa ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kwa Mwaka 2024 iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma leo Februari 07, 2025
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga akiwasilisha Taarifa ya shughuli za Kamati hiyo kwa mwaka 2024 bungeni jijini Dodoma leo Februari 07, 2025.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati wa Kikao cha Tisa cha Mkutano wa 18 wa Bunge jijini Dodoma leo Februari 07, 2025.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (kulia) akishiriki Kikao cha Tisa cha Mkutano wa 18 wa Bunge jijini Dodoma leo Februari 07, 2025. Kushoto ni Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akifuatilia Kikao cha Tisa cha Mkutano wa 18 wa Bunge jijini Dodoma leo Februari 07, 2025. Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dustan Kitandula.
………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema Serikali imeyapokea na inaendelea kuyafanyia kazi mapendekezo matatu ya mabadiliko ya Sheria ya Mazingira sura 191.
Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kanuni ya kulifanya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwa Mamlaka, umuhimu wa kutunga Sheria ya Uchumi wa Buluu na kutambuliwa kisheria kwa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC).
Mhandisi Masauni amesema hayo wakati akichangia Taarifa ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kwa Mwaka 2024 iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga bungeni jijini Dodoma leo Februari 07, 2025.
Waziri Masauni ameipongeza Kamati hiyo kwa mchango wake na kusema kuwa ni wenye maono katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya uhifadhi wa mazingira na kusisitiza kuwa dhamira ya Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais ni kuyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na Kamati hiyo.
“Kama ambavyo tuliwaahidi kwenye kamati, Mheshimiwa Spika naomba mbele yako niahidi tutayafanyia kazi yale yote mliyotushauri wakati wa michango ya wabunge na taarifa ya kamati, tayari tumeandaa mpango kazi kabambe ambao
mpaka leo tunavyozungumza hakuna hata kipengele kimoja hatujakitekeleza kama tulivyojipangia kwa hiyo tunakwenda vizuri,” amesema.
Mhandisi Masauni amesema kuwa ni matamanio ya Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kuona maeneo hayo matatu yaliyoainishwa ikiwezekana Bunge lijalo kwa ushirikiano mkubwa lipitishe.
Awali, akiwasilisha taarifa hiyo Mhe. Kiswaga amesema azimio la Bunge kuwa Serikali itoe mafunzo kwa wataalamu wa ndani wawe na ujuzi wa kuandaa mapitio ya tathmini ya athari kwa mazingira limetekelezwa kikamiulifu.
Mhe. Kiswaga ambaye pia ni Mbunge wa Kalenga amesema Ofisi ya Makamu wa Rais katika kipindi cha Februari hadi Desemba 2024 imetoa mafunzo hayo kwa jumla watumishi 75.
Pia, amesema azimio la pendekezo la kufanyia marekebisho ya Sheria ya Mazingira sura ya 191 ili iweze kuendana na Sera ya Taifa ya Mazingira 2021 ambapo Serikali iliwasilisha muswada wa marekebisho ya Shereia ya Mazingira
sura ya 191 ili kutatua changamoto za mazingira, imetekelezwa kwa kiasi fulani
hivyo kamati imesisitiza ikamilishwe. Kwa hatua hiyo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea na kukubali taarifa ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira