TEKNOLOJIA YA CRISPR-CAS9, HAITOI MADHARA HATA IKIMWAGILIWA NDOO YA DAMU YA UKIMWI

 Mwandishi Wetu,

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, ametoa maelezo ya kina kuhusu ufanisi wa teknolojia ya CRISPR-Cas9 na uwezo wake mkubwa katika matibabu ya magonjwa sugu na ya kurithi, akieleza kuwa teknolojia hiyo inafanya uhariri wa jeni kwa usahihi mkubwa na haithiri maeneo mengine ya mwili.

Akijibu maswali ya Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mhe. Askofu Dkt. Josephat Gwajima, aliyetaka kujua, ni lini Serikali itaanza kutumia teknolojia ya CRISPR-Cas9 katika matibabu ya magonjwa ya selimundu, ambapo Dkt. Mollel amesema kuwa teknolojia hiyo ina uwezo wa kuhariri jeni kwa usahihi, na inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kutibu magonjwa ya kurithi kama vile selimundu.

Amesisitiza kwamba hata katika hali isiyokuwa ya kawaida, kama vile iwapo CRISPR-Cas9 itamwagiwa na ndoo ya damu ya HIV, haitawaathiri wala kuleta madhara kwenye Gene nyingine.

"Teknolojia ya CRISPR-Cas9 inafanya kazi kwa umakini mkubwa na usahihi. Hata ikiwa itamwagiliwa ndoo ya damu ya HIV, haitakuwa na madhara yoyote kwa Gene nyingine au maeneo mengine ya mwili, inathibitisha ufanisi wake mkubwa na salama katika matibabu," amesema Dkt. Mollel.



Post a Comment

Previous Post Next Post