DKT. TULIA AKOSHWA NA MAJIBU YA KITAALAM YA WIZARA YA AFYA

 Na WAF, DODOMA,

Spika wa Bunge, Mhe. Tulia Ackson, amekubali uwezo wa kitaalamu wa Wizara ya Afya baada ya Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, kutoa majibu ya kina kuhusu matumizi ya teknolojia ya CRISPR-Cas9 katika matibabu ya magonjwa ya Seli mundu.

Katika majibu yake ya swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mhe. Askofu Josephat Gwajima aliyehoji wizara imejiandaaje kuleta muswada Bungeni ili kuleta sheria maalum itakayoongoza watu waofanyiwa Gene Editing, Dkt. Mollel ameeleza jinsi teknolojia ya CRISPR-Cas9 inavyoweza kufanya uhariri wa jeni (gene editing) kwa usahihi mkubwa bila kuathiri maeneo mengine ya mwili. Amefafanua kuwa teknolojia hii ni ya kisasa na inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kutibu magonjwa ya kurithi, yakiwemo magonjwa ya seli mundu.


Post a Comment

Previous Post Next Post