TUKO SALAMA KWA AJILI YA RAIS DK SAMIA ,HESABU ZAKE NI KALI SANA

 Mwandishi Wetu,

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amewatoa hofu wabunge kuhusu matumizi ya teknolojia ya CRISPR-Cas9, akisema kwamba Tanzania iko salama chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. 

Akizungumza Bungeni, Dkt. Mollel amesema kuwa Rais Samia ameweka mazingira bora ya maendeleo, hususan katika sekta ya afya, kwa kuwekeza katika teknolojia na mifumo bora inayolinda afya ya wananchi. 

 “Hesabu za Dkt. Samia ni kali, tuko salama kutokana na uwezo wake wa kutafakari na kuendana na teknolojia,” ameongeza Dkt.Mollel.

Dkt. Mollel ameeleza kuwa Rais Samia ni kiongozi imara na mwenye uwezo mkubwa wa kutafakari na kuendana na teknolojia mpya, hivyo hakuna haja ya wasiwasi kuhusu usalama wa taifa katika suala hili.

Pia, Dkt. Mollel amesisitiza kwamba Rais Samia amepambana kwa nguvu kuhakikisha kwamba Tanzania inapata mafanikio katika sekta ya afya na ndiyo maana amepata nishani ya "The Goalkeeper" kutokana na juhudi zake kubwa katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Haya yamejiri kufuatia swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mhe. Askofu Josephat Gwajima, akitaka kujua jinsi Serikali inavyohakikisha kuwa matibabu ya kutumia teknolojia ya CRISPR-Cas9 hayataathiri DNA za watu au kuwa na madhara kwa vizazi vijavyo.



Post a Comment

Previous Post Next Post