Mwandishi Wetu,
Watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) wametakiwa kuongeza weledi na ufanisi katika kutatua changamoto za wakulima ili kuhakikisha maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
Hayo yamesemwa leo, Januari 31, 2025, na Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo, wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika Morogoro. Dkt. Diallo amesisitiza umuhimu wa kutathmini mafanikio, kuweka vipaumbele vya kimkakati, na kuwa proactive katika utendaji kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent, amesema kikao hicho kimelenga kujadili utekelezaji wa bajeti ya 2024/2025 na mapendekezo ya bajeti ya 2025/2026, huku kikipokea maoni muhimu ya kuboresha huduma kwa wakulima.
✅ Ufanisi katika sekta ya mbolea ni nguzo muhimu kwa kilimo endelevu! 🌾💪