BODI YA TMA YAJENGEWA UWEZO KUBORESHA UTAENDAJI NA UZINGATIAJI WA MIJADALA YA TABIANCHI

 

Katika juhudi za kuboresha utendaji na kuimarisha usimamizi wa masuala ya hali ya hewa na tabianchi, Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepatiwa mafunzo maalum ya uongozi na usimamizi wa taasisi na Taasisi ya Uongozi. Mafunzo hayo ya siku mbili yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF, Jengo la Millennium II, Jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 29 hadi 30 Januari 2025.

Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Mh. Jaji Mshibe Ali Bakari, aliyefungua rasmi mafunzo hayo, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na uwazi katika kuhakikisha taasisi hiyo inafanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Katika muendelezo wa mafunzo hayo, Bodi ilifanya ziara katika mradi wa ofisi ya Kanda ya Mashariki na Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Tsunami, ambapo Katibu wa Bodi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a, aliishukuru Bodi kwa ziara hiyo na kwa miongozo itakayohakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi.

Mafunzo hayo yalijumuisha Bodi na Menejimenti ya TMA, ambapo mada mbalimbali zilitolewa, zikiwemo uongozi bora, uongozi wa kimkakati, na vihatarishi vinavyoweza kukwamisha ufanisi wa taasisi. Mafunzo haya yanatarajiwa kusaidia kuboresha utendaji wa TMA katika utoaji wa taarifa za hali ya hewa na kusaidia taifa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post