Katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetoa miche ya miti 2,000 kwa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) 303 KV, Arusha ili kuweza kuboresha utunzaji wa mazingira.
Miti hiyo iliyotolewa kwenye kitalu cha miti kinachosimamiwa na NCAA, inatarajiwa kupandwa na JWTZ kwenye maeneo mbalimbali Wilayani Monduli, Arusha.
Maadhimisho ya siku hii ya uhuru hufanyika kila mwaka tarehe 9 Disemba, ambayo kwa mwaka huu ni maadhimisho ya Miaka 63 tangu kupatikana kwa Uhuru wa Tanzania bara ikiwa na kauli mbiu isemayo "_Uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa Maendeleo yetu".