Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amekutana na wana-jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uingereza

 

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amekutana na wana-jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uingereza (Diaspora) katika mji  wa London baada ya kuwasili Disemba 08, 2024 na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya afya nchini Tanzania. 

Miongoni mwa mambo waliyojadiliana katika kikao hicho ni pamoja na dhana ya umuhimu wa Bima ya Afya kwa Wote, kuimarisha uendelezaji wa wataalam katika ngazi ya bingwa na ubingwa bobezi na kufungua fursa za wataalam wa afya kupata ajira nje ya nchi. 

"Vilevile tumejadiliana kuhusu kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya ikiwa ni pamoja na vifaa tiba na dawa, kuimarisha huduma za mkoba nchini kwa kufanya kambi mbalimbali za huduma za kibingwa kwa kutumia madaktari kutoka Uingereza na maeneo mengine," amesema Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amesisitiza umuhimu wa wana Diaspora hao kuendelea kushiriki kikamilifu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini Tanzania. ‎ 

Post a Comment

Previous Post Next Post