Kamishina Mkuu wa Malaka ya Mapato Tanzania, Yusuph Mwenda akizungumza akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati kamati hiyo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), walipotembelea Bandari ya Dar es Salaam, leo Desemba 4, 2024 na kuona ufanisi katika ufanyaji kazi wao.
Mkuu wa Idara ya y Masuala ya Kampuni ya Adani Ports Tanzania Donald Talawa akitoa taarifa ya shughuli zao mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati kamati hiyo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), walipotembelea Bandari ya Dar es Salaam, leo Desemba 4, 2024 na kuona ufanisi katika ufanyaji kazi waoMeneja Masuala ya Kampuni wa DP World Tanzania, Elitunu Mallamia, akitoa taarifa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, akielezea masuala mbalimbali yanayohusiana na shughuli za kampuni hiyo, wakati kamati hiyo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), walipotembelea Bandari ya Dar es Salaam, leo Desemba 4, 2024 na kuona ufanisi katika ufanyaji kazi wao
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Oran Manase akizungumza wakati kamati hiyo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), walipotembelea Bandari ya Dar es Salaam, leo Desemba 4, 2024 na kuona ufanisi katika ufanyaji kazi wao
Wabunge Wasifu Ufanisi Bandarini, Washauri Uwekezaji Zaidi
Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, imeridhishwa mabadiliko ya utendaji katika bandari ya Dar es Salaam na kusema yanaleta hamasa ya kuongeza magati, ili meli nyingi zaidi zihudumiwe kwa wakati mmoja.
Wajumbe wa kamati hiyo wameyasema hayo leo Desemba 04, 2024 walipotembelea bandarini na kuona ufanisi katika ufanyaji wa kazi hususani katika mapato na kupunguza siku za meli kusubiri kuingia nangano.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Oran Manase, amesema kamati hiyo itashauri serikali waweze kupanua miundombinu ili kuongeza wigo kwa wawekezaji wa bandari kwani itasaidia kuongeza ufanisi na kuufanya uwekezaji kuwa wenye tija.
"Lengo ni kuondoa vikwazo ili isionekane serikali ni kikwazo kwa wawekezaji wanaotaka kufanya kazi nchini
“Ili tufanye vizuri zaidi inabidi kuwa na maboresho kwenye miundombinu ya nje, tuongeze magati wenzetu wanamagati 20 mpaka zaidi ya 25 sisi tuna magati 11...kwa hiyo tuangalie ni namna gani ya kubalansi hayo magati.” Amesema Manase.
Ameongeza: “ Mizigo inayokuja sasa hivi unatupa hamu kwamba tunaweza kuongeza magati ili tusisubiri tena SGR italishwa na kuendeshwa na bandari.” amesema Manase
Aidha, amesema uwekezaji huo umeleta manufaa makubwa kwa kuangali kupungua kwa idadi ya siku za kusubiri bandarini kutoka siku 25 hadi siku mbili, hivyo alisema kuongezeka kwa wigo wa miundombinu kutasaidia kuongeza ufanisi zaidi na nchi za kuhudumia kutokana na uharaka utakaofanyika katika njia za usafirishaji.
Amesema uamuzi wa serikali kuleta wawekezaji hao katika bandari kumeleta tija kwani kumesaidia kuweka ajira kwa wazawa, kuongeza mapato kutokana na ukusanyaji wa kodi na kupunguza matumizi, hivyo alisema mapendekezo yao hayatokuwa na pingamizi kwani hayaleti wasiwasi.
Kwa upande wa Meneja wa Masuala ya Ushirika wa DP World, Elitunu Mallamia amesema wanahudumia shehena kuanzia gati namba sifuri hadi saba.
Amesema gati namba sifuri na moja zinapokea meli za magari, namba mbili hadi nne ni gati ya mizigo ya kichele yaani malighafi na gati namba tano hadi saba ni kwa ajili ya kuhudumia makasha.
“TPA ni mwenyenyumba wetu sisi ni waendesha gati, sisi tunahitaji msaada mkubwa kwenye maeneo yatakayotuwezesha kuhudumia na kusafirisha kwa haraka zaidi tuweze kupata ushirikiano kwa sababu ukubwa wa bandari unaathiri ushirikiano wetu kama nchi katika kuhudia shehena,” amesema Mallamia.
Pia amesema wanaomba maboresho kwenye miundombinu mingine tofauti na barabara yaani reli ili waweze kusafirisha mizigo kwa kasi zaidi.
Ameongeza toka waanze kazi wameweza kushusha idadi ya meli zinazosubiri hadi moja tofauti na ilivyokuwa awali na kuongeza kasi ya ushushaji wa magari kwa kutoka wastani wa magari 14,000 hadi magari 17,000 kwa mwezi.
Meneja wa Masuala ya Ushirika wa TEAGTL, Donald Talawa, amesema wao wanahusika kuhudumia nchi sita hadi nane na asilimia 55 ya wanaowahudumia ni mizigo ya watanzia na asilimia 45 ni kutoka nchi zinazozunguka Tanzania.
Pia amesema wao wanahudumia gati namba nne hadi nae na wanajishughulisha zaidi na kuhudumia meli za makontena na kuongeza kuwa wateja wao wakubwa ni Kongo na Zambia na kwa upande uganda wamekuwa wakiwahudumia kwa kiasi kidogo kutokana na changamoto ya miundombinu.
Amesema kwa upande wao wanaomba ufanisi uongezeke katika kuboresha mifumo na kuifanya mifumo iwe inayosomana ili kuweza kutoa mizigo kwa haraka kwenye bandari kwani kutosaidia kuongeza uwezo wao kwenye kuhudumia shehena zaidi ya wanavyofanya sasa.
Baada ya kutoka bandarini kamati hiyo ilitembelea Ofisi ya Mamlaka ya Mapato(TRA) iliyozibduliwa kwa ajili ya walipa kodi binafsi na wa hali ya juu Kamishna Jenerali wa TRA, Yusuph Mwenda alisema ofisi hiyo kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.
"Muunganiko huu na matoke haya ni kutokana na muundo mpya uliotengenezwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais Samia Suluhu Hassan, ofisi hii itakuwa ikihudumia makundi manne ambayo ni wamiliki wa makampuni makubwa yanayozalisha zaidi ya shilingi bilioni 20 kwa mwaka, wamiliki wa hisa zenye thamani ya shilingi bilioni 2.5 kwa mwaka,” ameeleza Mwenda.