WAZIRI MKUU AWATAKA WAFAMASIA KUHESHIMU MAADILI, KUFUATA TARATIBU ZA UTOAJI DAWA

 Na, WAF-Dodoma, 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amewataka wafamasia nchini kuzingatia maadili ya taaluma yao na kuhakikisha dawa zinatolewa kwa kufuata taratibu, ikiwa ni pamoja na kutokutoa dawa bila cheti cha daktari.

Akizungumza leo Disemba 04, 2024 jijini Dodoma wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa 54 wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST), Waziri Mkuu ameeleza kuwa hatua za kudhibiti matumizi holela ya dawa ni muhimu katika kulinda maisha ya wananchi na kujenga imani ya jamii kwa huduma za afya.

“Ni jukumu la kila mfamasia kuhakikisha dawa zinatolewa kwa kufuata taratibu sahihi. Kutoa dawa bila cheti cha daktari kunahatarisha maisha na kuharibu maadili ya taaluma hii muhimu,” amesema Mhe. Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu ameielekeza Wizara ya Afya kupitia upya kanuni zinazohusu uendeshaji wa maduka ya dawa yaliyopo pembezoni mwa hospitali, akisisitiza kuwa ni muhimu kuwepo utaratibu unaoruhusu uuzaji wa dawa katika maeneo hayo, huku hatua za kudhibiti wizi wa dawa na uvunjifu wa sheria zikizingatiwa.

Mhe. Majaliwa pia ameagiza waajiri wote wa sekta ya afya kuhakikisha kuwa wafamasia waliopo kazini, ambao ni wanachama wa PST, wanapewa ruhusa ya kushiriki mikutano ya chama hicho bila vikwazo.

Aidha, Mhe. Majaliwa amewaasa wananchi kuacha matumizi holela ya dawa na badala yake wafike katika vituo vya kutolea huduma za afya na kupima kisha kutumia dawa stahiki inayotakiwa badala ya kutumia dawa bila ya kujua nini tatizo



Post a Comment

Previous Post Next Post