MGODI WA STAMIGOLD BIHARAMULO WASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA

 

Kampuni ya STAMIGOLD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kupitia mgodi wake wa Stamigold Biharamulo uliopo wilayani Biharamulo mkoa wa Kagera umeshiriki katika Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika eneo la Butulwa Old Shinyanga Mkoani Shinyanga.
 
Kilele cha Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini yaliyoongozwa na kauli mbiu ya ‘Biashara na madini ni chachu ya maendeleo Shinyanga’ kimefanyika Disemba 1,2020 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kikula. 
 
Akizungumza kwenye maonesho hayo, Meneja Mkuu wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika, alisema mgodi huo unakabiliwa na gharama kubwa ya uzalishaji wa madini ya dhahabu hivyo kuishukuru serikali kwa kuwaunganishia huduma ya umeme kutoka Kituo cha Geita na hatua iliyofikiwa ,inatarajiwa umeme kuanza kutumika Februari 2021 ambapo kwasasa Mgodi unatumia genereta za dizeli.
 
“Tangu mgodi huu uwe chini ya Serikali mwaka (2014), na kuanza uzalishaji rasmi 2015, umekuwa ukiingia kwenye gharama kubwa ya kutumia Genereta na mafuta ya Diesel  yenye gharama za Shilingi Bilioni 1.2 kwa mwezi na endapo tutapata huduma ya umeme gharama itapungua na tutatumia shilingi Milioni 300”,aliongeza Meneja Mkuu wa Mgodi , Mhandisi Gilay Shamika.
 
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Prof. Idris Kikula akiwa kwenye Banda la Mgodi wa StamiGold Biharamulo, aliupongeza mgodi huo kwa kufufuka tena na kuanza uzalishaji wa madini akieleza kuwa faida imekuwa ikipanda kila Mwaka na kusaidia STAMICO kulipa gawio Serikalini.
 
“Endeleeni kama mnavyofanya ila kwenye ushirikiano na wananchi tumieni mkataba katika kutekeleza maendeleo endelevu na vijijini (CSR)”, alisema Prof. Kikula.

 

Kulia ni Meneja wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika, akimuelezea  Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula (katikati aliyevaa miwani) namna mgodi huo unazalisha madini ya dhahabu alipotembelea Banda la Stamigold kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini eneo la Butulwa Old Shinyanga mkoani Shinyanga Disemba 1,2020. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kushoto ni Meneja wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika, akimuelezea  Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula (wa pili kulia) namna mgodi huo unazalisha madini ya dhahabu alipotembelea Banda la Stamigold kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini eneo la Butulwa Old Shinyanga mkoani Shinyanga
Meneja wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika, akimuelezea  Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula (wa pili kulia) namna mgodi huo unazalisha madini ya dhahabu

 

Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Prof. Idris Kikula akizungumza kwenye Banda la Mgodi wa StamiGold Biharamulo, na kuupongeza mgodi huo kwa uzalishaji wa madini wakati wa maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga Disemba 1,2020.

 

Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Prof. Idris Kikula akizungumza kwenye Banda la Mgodi wa StamiGold Biharamulo, na kuupongeza mgodi huo kwa uzalishaji wa madini wakati wa maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa Shinyanga Disemba 1,2020
 
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Post a Comment

Previous Post Next Post