SIKU YA MBOLEA DUNIANI 2024, KUADHIMISHWA MJINI BABATI,DODOMA

 Mwandishi Wetu,

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Joel Laurent, amesema mazingira wezeshi ya uwekezaji katika tasnia ya Mbolea nchini yanayofanywa na Serikali, yanaendelea kuchochea uzalishaji wa ndani wa mbolea na visaidizi vyake hivyo kuongeza uhakika wa upatikanaji wa mbolea nchini.

Mkurugenzi huyo amesema hayo leo katika mkutano na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali makao makuu ya TFRA jijini Dar es salaam, katika kuelekea maadhimisho ya siku ya mbolea duniani, yatakayofanyika kuanzia Oktoba 10 na kuhitimishwa Oktoba 13 mwaka huu mjini Babati Mkoani Manyara.

Amesema kuwa kwasasa viwanda vya uzalishaji wa mbolea nchini na visaidizi vyake vimeongezeka hadi kufikia 23, ambapo kati ya hivyo viwanda vitatu ni vikubwa, vinavyoendelea kuchochea ongezeko la uzalishaji wa ndani na kuongeza uhakika wa upatikanaji wa mbolea nchini na tija ya uzalishaji.

Akizungumzia maadhimisho ya siku ya mbolea duniani nchini Tanzania Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa, mwaka huu yataadhimishwa tofauti katika kuipa umuhimu zaidi siku hii muhimu kwa wadau wa mbolea nchini.

Amefafanua kuwa licha ya maonesho ya mbolea yatakayofanyika mjini Babati katika viwanja vya stendi ya zamani, pia TFRA imeandaa kongamano kubwa la kwanza la Mbolea la aina yake litakalowakutanisha wadau wa mbolea kutoka ndani na nje ya nchi, kujadili kwa Pamoja tasnia ya mbolea, ambapo kongamano hilo litafanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Oktoba 11 na 12 katika shamra shamra za maadhimisho ya siku ya mbolea duniani.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa kutakuwa na mbio za ridhaa siku ya kilele Pamoja na burudani mbalimbali kunogesha kilele cha siku ya mbolea duniani mjini Babati, na kuwaomba wadau kujitokeza kwa wingi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ruzuku taifa na kaimu mkurugenzi wa uzalishaji wa ndani na ununuzi wa mbolea kwa Pamoja Louis Kasera, amesema kuwa uwepo wa mpango wa mbolea ya ruzuku umeongeza kiasi cha matumizi sahihi ya mbolea na kuchochea tija ya mavuno nchini.

Aidha amewakumbusha wakulima kuendelea kujisajili kwenye daftari la mkulima na kwenye mfumo wa kidigitali wa mbolea ya ruzuku ili kuendelea.




Post a Comment

Previous Post Next Post