IDARA YA FORODHA TRA WATETA NA WASAMBAZAJI VING'AMUZI

 Kaimu Naibu Kamishna wa Forodha wa TRA, Juma Hassan akizungumza wakati wa kuzindua mkutano na mawakala wa forodha pamoja na mawakala wa Ving'amuzi leo jijini Dar es Salaam.






Baadhi ya Washiriki wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) idara ya forodha.


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Idara ya Forodha leo Juni 29, 2024 Wakutana na Wasambazaji wa Ving'amuzi Tanzania ili kuhakikisha mizigo yote inakwenda nje ya nchi bila kubaki nchini.

Akimwakilisha kamishna wa Forodha,  Felix Tinkasimile,  Kaimu Naibu Kamishna wa Forodha wa TRA, Juma Hassan amesema kuwa kufika katika ukumbi huo wanana nia nzuri sio tuu kwa mamlaka bali na hata kwa washiriki binafsi.

"Tupo hapa kuhakikisha kwamba tunawapa elimu, pia tunabadilishana uzoefu v kuona changamoto zipo wapi na wapi wasimamie vizuri."

Amesema kuwa watakwenda kuangalia Mafanikio, changamoto pamoja na maono ya pamoja kwaajili ya kuboresha ufanisi na usalama na ushindani wa Bandari.

Amesema kwa kupitia utekelezaji wa mpango wa Authorized Economic Operators (AEO) pamoja na utekelezaji wa mfumo wa kieletroniki uliofungwa kwaajili ya kuangalia namna Malori yanayosafirisha mizigo kwenda nje ya nchi.

"Naomba kuwasisitizia umuhimu wa AEO kwa mazingira ya sasa ni muhimu katika utekelezaji wake."

Kwa upande wa Meneja wa Usimamizi wa Usafirishaji Mizigo kutoka Makao Makuu ya Forodha Paul Kamkulu, amesema kuwa wapo tayari kuhakikisha kwamba tunashirikiana katika eneo la forodha na serikali ambapo serikali inaweza kuchukua kitu ambacho ni cha kwake bila kumwonea mtu yeyote.

"Lakini kuhakikisha kwamba watu wa nchi nyingine wanachukua mizigo yao kwenye mipaka yetu kwa kufuata taratibu zote za kiforodha." Amesema

Amesema kuwa wamewaita wenzao wasafirishaji wa Mizigo na Mawakala wa kusambaza Ving'amuzi vya forodha ili waweze kusimamia mizigo ya forodha kwenda nje ya nchi.

Katibu wa Chama cha Wafunga Ving'amuzi,

Francis Mkini amemshukuru kamishna wa forodha kwakutambua mchango wao wa kudhibiti nakuhakikisha kwamba mizigo inafika sehemu iliyokusudiwa kwa muda stahiki na kwa usalama.

"Uongozi wa TRA kwa kupitia kwa Kamishna wa Forodha na kutujumuisha katika kudhibiti ubora wa ufikaji wa mizigo kwanamna ambayo imekusudiwa, kwa kiasi kilichokusudiwa na kwa muda stahiki na ulipaji kodi unakuwa kwa asilimia zile zilizokusudiwa mwisho mafanikio hayo yatapelekea kodi kukusanywa katika kiwango ambacho nichajuu ukilinganisha na wakati ambapo kulikuwa hakuna mawakala ambao wakufunga ving'amuzi na kudhibiti ufikaji wa mizigo na kuepuka kutokufika kwa mizigo nchi husika.

"Jambo hili litajenga msingi mzuri wa Uboreshaji wa serikali yetu katika maendelo kutokana na mapato yanayotokana na kodi.

Post a Comment

Previous Post Next Post