WAONGOZA WATALII HAPA NCHINI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA PAMOJA NA KUTANGAZA VIVUTIO VILIVYOPO TANZANIA

 Na Pamela Mollel,Arusha


Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili na utalii Dkt Hassan Abbas amewataka waongoza utalii hapa nchini kutoa huduma bora za utalii pamoja na kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania

Dkt,Abbas aliyasema hayo jijini Arusha wakati akifunga semina kwa waongoza utalii,akimwakilisha Waziri wa wizara hiyo Mohamed Mchengerwa

Alisema kuwa vivutio vilivypo nchini lazima vitangazwe ili wageni wa ndani na nje ya nchi waweze kuvifikia vivutio hivyo

"Kama tunavyojua waongoza watalii ni mabalozi namba moja katika kutangaza utalii hapa nchini basi tufanye kazi hii kifua mbele maana Rais Samia Suluhu Hassan amewaheshimisha sanaaa waongoza utalii kupitia Filamu maarufu ya Royal tour "alisema Abbas

Alisema kupitia filamu ya Royal Tour watu bilioni 1.2 wameiona na kuijua nchi ya Tanzania ilivyo na vivutio vingi vya utalii na hii filamu imeanza kuleta watalii wengi nchini ikiwemo waongoza watalii kupata kazi nyingi zaidi

Naye Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA),William Mwakilema alisema Tanapa imejipanga kutangaza hifadhi tano ikiwemo Hifadhi ya Mkomazi ambayo awali zilikuwa hazitangazwi sana katika sekta hiyo ya Utalii

Alizitaja hifadhi nyingine ambazo ni Saadani,Mikumi,Nyerere na Ruaha ambazo zimekuwa hazijulikani sana hivyo Tanapa imedhamiria kuzitangaza zaidi na kuziweka kwenye vifurushi vya safari za waongoza utalii nchini

Alisema utaratibu wa kufanya utalii katika vivuko vya nyumbu nakuazimia kwa pamoja waongoza utalii kuzingatia sheria na kanuni ikiwemo usafi wa mazingira kwa kwakushirikiana Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Tanapa na wadau mbalimbali wataandaa vipeperushi maalum vya kutunza mazingira.

Alisema kampeni yao ya" Discover Mkomazi " itazinduliwa muda wowote kuanzia sasa yenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii ambavyo havijatangazwa sana na kuagiza Tanapa kutoa mafunzo ya lugha zaidi za watalii kulingana na mataifa ya watalii wanaokuja nchini Tanzania "

Naye Mwakilishi wa Waongoza Watalii Tanzania,Ridas Maiko Laizer amesema semina hiyo iliyoshirikisha waongoza utalii zaidi ya 1,302 ni chachu ya kuongeza idadi ya watalii milioni 5 ifikapo 2025 ambapo pia waliomba waongoza watalii hao kupata mikataba ya kazi ikiwemo viwango maalum vya malipo.

Pia maslahi ya waongoza watalii kiwango kisiwe chini ya dola za marekani 5O kwa siku kwani kampuni nyingi za utalii zinawatoza watalii fedha hizo lakini chaajabu waongoza utalii hawapewi fedha hizo lakini pia leseni za wangoza utalii wanaomba zifutwe kwani ajira hiyo si rasmi

Aliomba vitambulisho vya vyama vya utalii vitumike badala ya vile vya makampuni na waliiomba serikali kuongeza kiwango cha fedha za bima ya Afya ili wanapoumwa waweze kutibiwa kuliko kuingia gharama kubwa za matibabu na kusisitiza wamiliki wa mahoteli watoe vipaumbele katika huduma za malazi ili nao waweze kulala mahali pazuri badala ya watalii pekee kulala ndani ya hoteli hizo.




Post a Comment

Previous Post Next Post