JKCI na Yanga kushirikiana kufikisha elimu ya magonjwa ya moyo katika jamii

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga Andre Mtine wakibadilishana hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya Yanga baada ya kusaini hati hizo leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

Afisa Mtendaji wa Mkuu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga Andre Mtine akimpatia jezi ya klabu hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuonesha moja ya wodi za VIP Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga Andre Mtine mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akimuelezea hali ilivyo katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga Andre Mtine mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya mpira wa miguu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga Andre Mtine akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Klabu ya mpira wa miguu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa klabu ya mpira wa miguu ya Yanga na wafanyakazi wa JKCI mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua matikio ya picha wakati wa kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam

Picha na JKCI

******************************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga zimesaini hati ya mkataba wa ushirikiano katika utendaji wa kazi na kuielimisha jamii kuhusu magonjwa moyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge alisema JKCI ndio taasisi pekee inayotoa huduma za upasuaji wa moyo nchini na ya tatu kwa ukubwa Barani Afrika katika kutoa huduma za matibabu ya moyo pamoja na upasuaji wa moyo.

Pamoja na kusaini mkataba huo Dkt. Kisenge pia ametoa ofa kwa mashabiki wa timu hiyo wenye kadi za uanachama kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo kwa punguzo la asilimia 20 katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

“JKCI imekuwa ikitoa huduma kwa wagonjwa zaidi ya 900 kwa siku na kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 700 kwa mwaka ambapo asilimia 20 ya upasuaji wa huo unaofanyika kwa watoto wadogo ambao wengi wao wanatoka katika familia masikini zisizokuwa na uwezo wa kugharama matibabu ya moyo”, alisema Dkt. Kisenge

Dkt. Kisenge alisema JKCI kuungana na klabu ya Yanga kuna faida kwani kupitia klabu hiyo JKCI itafahamika zaidi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa wachezaji wa timu hiyo kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo.

“Serikali yetu inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inachangia asilimia 70 katika matibabu ya watoto wetu na asilimia 20 inayobaki tunasema kuwa hatutaki mtoto hata mmoja anayefika JKCI akose matibabu ndio maana tunaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo klabu ya Yanga”, alisema Dkt. Kisenge

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine alisema JKCI imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji huduma za matibabu ya moyo hivyo Klabu ya Yanga ikaamua kuchukua jukumu la kuwa sehemu ya JKCI kuhamasisha jamii kujitokeza kupima na kuitangaza JKCI ndani na nje ya nchi.

“Kila mtu anajua yakuwa taifa lililo na afya bora ni taifa lililo na furaha hivyo kutokana na sababu hiyo ndio maana sisi Yanga tumeamua kuungana na JKCI kuhamasisha jamii kuwa na afya bora”, alisema Andre

Andre alitoa wito kwa wanachama wa klabu ya Yanga kuhakikisha wanapata kadi za uanachama ili waweze kupata ofa iliyotolewa na JKCI ya kupatiwa huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya moyo.

“Klabu ya Yanga itashiriki katika usiku wa dinner gala unaoandaliwa na Taasisi kwa lengo la kuchangia matibabu ya watoto wanaotibiwa JKCI ili nasi tuwe sehemu ya kujenga Taifa lililo na furaha”, alisema Andre

Naye daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani alisema uelewa wa magonjwa ya moyo katika jamii umekuwa mkubwa na kuifanya jamii kutafuta matibabu pale tu inapoona dalili za magonjwa hayo.

“Wodi yetu ya watoto ina uwezo wa kulaza watoto 23 lakini kutokana na uhitaji kuwa mkubwa leo hii tuna watoto 48 ambao wengine tumewalaza katika wodi za watu wazima”, alisema Dkt. Naiz

Dkt. Naiz alisema kupitia wadau mbalimbali watoto wengi wamekuwa wakipatiwa huduma za upasuaji wa moyo lakini kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa kila wanapozaliwa watoto 100 kati ya mtoto 1 hadi 2 huzaliwa na tatizo la moyo hivyo kuendelea kufanya idadi ya watoto wanaosubiria upasuaji wa moyo kutopungua.

Post a Comment

Previous Post Next Post