Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya (kushoto) akikabidhi funguo za gari Toyota H/Top kwa Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Pareto Lucas Ayo leo jijini Arusha. Gari hiyo imekabidhiwa ili kusaudua bodi kuhamasisha wakulima wengi kulima zao la pareto nchini.Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pareto Lucas Ayo akionyesha funguo za gari mara baada ya kukabidhiwa leo toka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya (kushoto). Hafla hiyo ilifanyika jijini Arusha leo. Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akikagua shamba la mbegu bora za mahindi lililopo Ngaramtoni Arusha.Shamba hilo lenye ukubwa hekta 760 linamilikiwa na Wakala wa Mbegu (ASA). Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (katikati) akitoa maelekezo kwa dereva wa Bodi ya Pareto Venance Haule (kushoto) leo alipokabidhi gari kwa bodi hiyo jijini Arusha .Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (wa saba toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa wizara na taasisi zake zilizopo Arusha leo alipokabidhi gari kwa Bodi ya Pareto