Maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mkoani Morogoro na jijini Dar es Salaam ambapo kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kitaifa.
Jijini Dar es salaam maadhimisho yamefanyika kimkoa katika Uwanja wa Uhuru uliopo Wilaya ya Temeke.
Kauli mbiu kwa mwaka huu ni “Mishahara Bora na Ajira za Staha ni nguzo kwa maendeleo ya Wafanyakazi" Wakati ni Sasa!
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Mwanahamisi Munkunda, ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.