MOI YAFANYA MAFUNZO YA KUONGEZA UFANISI KATIKA UTOAJI HUDUMA

 

Na Mwandishi wetu- MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili -MOI imeendesha mafunzo maalumu kwa watoa huduma wake kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma za kibingwa.

Mratibu wa mafunzo hayo Dkt. Albert Ulimali amesema hii ni moja ya mkakati wa taasisi ya MOI wa kuhakikisha kila mwananchi anapatiwa huduma bora za kibingwa za MOI.

“Mafunzo haya kwa watoa huduma ni endelevu kwani leo tumeanza na watoa huduma kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na Idara ya Usingizi na Ganzi kwa lengo la kuboresha huduma zetu.

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Karima Khalid kutoka MOI amesema lengo la mafunzo haya ni kuhakikisha wafanyakazi wa MOI wanaweza kuendana na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowazuia kutokufanya kazi kwa ufanisi.

Naye Bw. William Astone ambaye ni mmoja wa aliyehudhuria mafunzo ameushukuru uongozi wa MOI kwani mafunzo haya yatawasaidia watoa huduma kukabiliana na msongo wa mawazo pamoja na uchovu unaoweza kupelekea utendaji wa kazi kushuka.

Post a Comment

Previous Post Next Post