Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais na Mazingira Selemani Jaffo akipa cheti Cha utambuzi katika masuala ya mazingira Diwani wa kata ya Kisutu Khery Kessy juzi (Picha na Heri Shaaban)
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisutu Elizabeth Masawe akimpa zawadi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais na Muungano Selemani Jaffo wakati wa siku ya kupanda miti shule ya Msingi Kisutu Ilala (Picha na Heri Shaban)
Maafisa Elimu Msingi wilaya ya Ilala wakiwa katika Picha ya Pamoja na Wanafunzi wa shule ya Msingi wakati wa tukio la Kupanda Miti shuleni hapo (Picha na Heri Shaban)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais na Mazingira Selemani Jaffo akipa cheti Cha utambuzi katika masuala ya mazingira Diwani wa kata ya Kisutu Khery Kessy juzi (Picha na Heri Shaaban)
……………………………….
Na Heri Shaaban, Ilala
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais na Muungano na Mazingira Selemani Jaffo ,amewataka Wakuu wa Wilaya nhini kupanda Miti Ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi kwa kupanda miti katika WIlaya zao .
Waziri Selemani Jaffo, alisema hayo Shule ya Msingi Kisutu Wilayani Ilala katika Kampeni endelevu ya Soma na Mti ambapo shule hiyo imepanda miti kwa ajili ya utunzaji Mazingira .
“Naagiza kwa Wakuu wa Wilaya wote tupande miti kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi Ili nchi yetu isiwe jangwa na kupelekea mfumuko wa Bei ya vyakula kama sasa mchele umepanda Bei tofauti na Bei za hapo awali ” alisema Waziri Jafo
Waziri Selemani Jaffo alisema Taifa lazima lipande miti hivyo Wakuu wa Wilaya wametakiwa kusimamia KAMPENI hiyo sambamba na kuwataka watoa vibari vya ujenzi kuwapa sheria kila unapojenga Nyumba lazima upande miti eneo lako kwa ajili ya suala Zima la utunzaji Mazingira .
Akizungumzia kampeni ya upandaji miti shule ya Msingi Kisutu alipongeza Uongozi wa shule ya Msingi Kisutu Mwalimu Mkuu Elizabeth Masawe , pamoja na Afisa Elimu Msingi Mwalimu Wilaya ya Ilala Siporah Tenga ambapo aliagiza kuendeleza Kampeni hiyo ya upandaji miti katika shule za Msingi Ilala kwa ushirikiano na Ofisi yake kwa ajili ya suala Zima la utunzaji Mazingira .
Alisema atamsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika suala zima la utunzaji Mazingira katika nchi yetu na kuwakikisha miti inapandwa eneo sehemu zote.
Aliwataka Watanzania wawe na upendo kwa ajili ya mafanikio ya Watu wote wapendane wapunguze mawazo wasije kuzeeka haraka .
Wakati huohuo amewewataka Watanzania kupendana na kuliombea Amani Taifa Letu na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt ,Samia Suluhu Hassan za kuleta maendeleo katika sekta Mbalimbali ,Ikiwemo Miundombinu ya Barabara ,Afya,Elimu reli ya kisasa SGR ,sekta kilimo na bwawa la kisasa la Mwalimu Nyerere .
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisutu Elizabeth Masawe ,alisema kampeni ya utunzaji miti wataendeleza na kuisimamia katika suala zima la utunzaji Mazingira na kuunga mkono Juhudi Rais Katika suala Zima la MAZINGIRA Katika shule ya Kisutu utakuwa endelevu .
Mwalimu Masawe alisema miti waliyoipanda wataitunza Katika shule yao na kuakikisha vizazi vijavyo wanakuja kuikuta .
Akizungumzia shule ya Msingi Kisutu alisema kwa Sasa Ina wanafunzi jumla 2016 wakiwemo wavulana 918 na wasichana idadi yao 1098 ambapo na idadi ya Walimu. 31 wanawake 28 na wanaume watatu .
Kwa upande wa kitaaluma shule ya Kisutu umekuwa ikifanya vizuri na kuongoza ufaulu wanafunzi hasa katka mitihani ya Taifa .
“Darasa la nne Katika Miaka mitatu kuanzia mwaka 2022,2021 mpaka mwaka 2022 matokeo ufaulu asilimia 100 na darasa la Saba kwa kipindi cha Miaka mitatu kuanzia mwaka 2020 mpaka 2022 ufaulu wanafunzi asilimia 100 wote wameenda kidato cha kwanza ” alisema Masawe